NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MBUNGE
wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka ameridhishwa na kasi ya
ujenzi wa upanuzi wa barabara ya njia nane kutoka Kimara-Kibaha kufikia
asilimia 59.1 na kudai kukamilika kwa barabara hiyo kuna kwenda kuinua
uchumi wa mji huo na kujibu changamoto ya msongamano wa magari.
Aidha
ameomba serikali na taasisi husika kuangalia umuhimu wa ombi lake la
kuomba ujenzi wa barabara hiyo awamu ya kwanza ivuke mji wa Kibaha ili
kuleta manufaa ya maendeleo ya mji huo unaoelekea kuwa manispaa ,kuliko
kuishia mwanzoni mwa Kibaha .
Akizungumza
wakati wa ziara yake ya kutembelea baadhi ya miradi kuonyesha wajumbe
wa halmashauri kuu ya CCM ,Kibaha Mjini utekelezaji wa ilani hasa miradi
ya kitaifa,kijimbo na kikata,Koka alisema, serikali inafanya kazi kubwa
kutatua changamoto za miundombinu ya barabara na sekta nyingine kwa
maslahi ya Watanzania.
"Barabara
hii inakwenda kupunguza msongamano na kuinua uchumi wa
Kibaha"tunashukuru kwa kasi anayokwenda nayo mkandarasi na nimpongeze
Rais dokta John Magufuli kwa jitihada zake kuelekeza nchi katika uchumi
wa kati"alielezea Koka.
Akitembelea
ujenzi wa hospital ya wilaya Lulanzi, kata ya Pichandege ,Koka alisema
fedha milioni 220 inayohitajika kukamilisha ujenzi huo itasaidia kuanza
kwa huduma haraka hivyo atalisimamia suala hilo.
Wajumbe
hao pia walipitia ujenzi wa soko la kisasa ,na mbunge huyo alibainisha
litakuwa ni kariakoo ya Kibaha kwani mahitaji yote yatapatikana mjini
hapo.
"Tangu
jimbo hili lianze ,haijawahi kutokea kuambatana na ujumbe huu mzito,
lakini nimesukumwa kutokana na kwamba halmashauri inapokea utekelezaji
wa ilani hivyo wamekuja kushuhudia utekelezaji huo ili wakirudi kwa
wananchi waweze kueleza serikali inafanya yapi makubwa ,"
Nae
mwakilishi wa meneja wa TANROADS Dar es salaam ,ambae ni msimamizi wa
barabara ya njia nane kutoka Kimara-Kibaha ,Issa Mbula alisema ujenzi wa
mradi huo,umefikia asilimia 59.1 na muda wa mradi umefikia asilimia 60
na utagharimu sh.bilioni 140 .
Akiongea katika mradi wa ujenzi wa hospital ya wilaya,mganga mkuu wa mji wa Kibaha, Dokta.Tulitweni Mwinuka alisema walipokea serikalini bilioni 1.5 na halmashauri milioni 290 lakini wanahitaji ziada ya milioni 220 ili kukamilisha ujenzi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...