Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha
Bw. Richard Kwitega akikagua bidhaa za wanawake wajasiliamali jana
Mkoani Arusha wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake
Kiuchumi linaloendelea Jijini Arusha kushoto kwake ni Mboni Mgaza
Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya familia kutoka Wizara ya Afya.

Mwanamke Mjasiliamali akifafanua
jambo kuhusu bidhaa ya wine inayotengenezwa kiwandani kwake kwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega wakati wa ufunguzi wa
Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi linaloendelea Jijini Arusha
kushoto kwake ni Mboni Mgaza Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya familia
kutoka Wizara ya Afya.

Baadhi ya wanawake walioshiriki
katika Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wakifutilia jambo
wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo jana Arusha.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha
Bw. Richard Kwitega akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake
wajasiliamali jana Mkoani Arusha mara baada ya ufunguzi wa Kongamano la
Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi linaloendelea Jijini Arusha.
………………………
Na Mwandishi Wetu Arusha
Serikali
inatambua kuwa haiwezi kufikia malengo ya maeandeleo endelevu ikiwa
wanawake hawatashiriki na kunufaika na uchumi kama ilivyo kwa wanaume
kwasababu mfumo dume hautoshi kuiletea Nchi maendeleo.
Hayo yamesemwa
leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega wakati wa
ufunguzi wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi linaloendelea
Jijini Arusha.
Bw. Kwitega
ameongeza kuwa ili kuwa na maendeleo endelevu ni lazima kuwashirikisha
wanawake kiuchumi ili kunuafaika na uchumi au matokeo ya shughuli za
Maendeleo.
Aidha Bw. Kwitega
aliongeza kuwa kwa kuzingatia dhamana ya Wizara ya Afya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii ya uratibu na wa masuala ya usawa wa kijinsia na
uwezeshaji wanawake kiuchumi inaendelea na maandalizi ya sera ya Jinsia
ili kuhakikisha mipango yote inazaingatia usawa wa kijinsia.
Bw. Kwitega
ameitaja mikakati na mipango ya maendeleo ya Taifa pamoja na mpango wa
Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kuwa mipango
yote iliyopo inaielekeza Serikali kuwezesha wanawake kiuchumi.
Kiongozi huyo wa
Mkoa wa Arusha amezija juhudi za serikali katika kuhakikisha wanawake
wanakua kiuchumi kuwa ni kuhamasisha wanawake kujiunga VICOBA na SACCOS
na vikundi vingine vya hisa na kuongeza kuwa mpaka sasa serikali ina
vikundi 918 venye jumla ya Wanawake 10,708 wamejiunga na vikundi hivyo
Nchi nzima.
Naye Mkurugenzi
Msaidizi Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Mboni Mgaza
amesema lengo kuu la Kongomano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ni
kuwatayarisha wanawake Mkoani Arusha pamoja na Taasisis
zinazojishughulisha na uwezeshaji wanawake kuweza kuwajenga uwezo wa
kiuchumi.
Bi. Mgaza
amezitaja mbinu zinazotumika kujengea uwezo wa wanawake kiuchumi ni
pamoja na kuwapa mitaji na mikopo lakini pia kuwapa ujuzi wa teknolojia
na kujenga ubia baina ya Serikali na Taasisi mbalimbali.
Bi. Mboni
aliongeza kuwa Kongamano hilo la wanawake linalenga vikundi vya
kiuchumi, vikundi vya ujasiliamali pamoja na watu binafsi zikiwemo
taasisi mbalimbali Mkoani Arusha kwa lengo la kupata maarifa mbalimbali
ya kujikwamua kiuchumi.
Serikali imekuwa
ikitoa Mikopo kupitia Serikali za Mitaa kwa Wanawake waliokatika vikundi
vya hisa na ujasiliamali kwa lengo kuwezesha wanawake kiuchumi na
tayari Serikali tayari kupitia mapato ya Halmashauri zote Ncini inatenga
asilimia kumi ya mapato yake kwa lengo la kuwezesha wanawake vijana na
walemavu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...