Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasha pikipiki kuashiria
uzinduzi wa zoezi la ugawaji pikipiki 15 kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii
katika Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu
wa mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Afisa Maendekeo ya
Jamii Mkoa wa Katavi Bw. Ignas Kikwala moja ya pikipiki 15 zilizotolewa
kwa Maafisa hao katika Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi kushoto ni
Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe.
Lilian Matinga.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa zoezi la ugawaji pikipiki 15 kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii katika
Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wa pili kushoto ni Mwakilishi wa
Mkuu wa mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga
na wa tatu kulia ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara ya Maendeleo ya
Jamii Bw. Julius Mbilinyi.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Wilaya
ya Tanganyika mkoani Katavi kabla ya kugawa pikipiki kwa Maafisa
Maendeleo ya Jamii ili ziwawezeshe kuwafikia wananchi na kuwasaidia
kutatua changamoto zao.

Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa
Katavi Mhe. Lilian Matinga akieleza mikakati ya mkoa katika kuhakikisha
wanaratibu Maafisa Maendeleo ya Jamii kuwafikia wananchi na kuwasaidia
kutatua changamoto zao wakati wa hafla ya ugawaji wa pikipiki kwa
Maafisaa hao kutoka Wilaya ya Tanganyika.

Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya
Tanganyika Mkoa wa Katavi wakimsikiliza Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati
wakizungumza nao katika hafla ya ugawaji pikipiki 15 kwa Maafisa
Maendeleo ya Jamii katika Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi.
…………………..
Na Mwandishi Wetu Katavi
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametoa pikipiki 15 kwa Maafisa
Maendeleo ya Jamii kutoka katika Kata za Wilaya ya Tanganyika mkoani
Katavi na kusisitiza matumizi mazuri na yaliyokusudiwa ya pikipiki hizo.
Akizungumza katika halfa ya
ugawaji pikipiki hizo Waziri Ummy Mwalimu amewataka Maafisa Maendeleo ya
Jamii nchini kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili
jamii ya Watanzania kwa kuhakikisha wanawasaidia kupata fursa za
kujiwezesha kiuchumi.
Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu
ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. John Pombe Magufuli imejikita katika
kuhakikisha inawasaidia wananchi kuondokana na umasikini kwa kuwezesha
kupata mikopo isiyo na riba kutoka katika Halmashauri ikiwa imelenga
kundi la wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
“Msizitumie pikipiki hizi kwa
mambo yenu binafsi na msizifanye bodaboda za biashara kazitumieni
kuwafikia wananchi na kuhakikisha mnatatua changamoto zao ili waweze
kujiletea maendeleo yao”
Aidha Waziri Ummy amezitaka
Halmashauri zote nchini kuendelea kutenga asilimia 10 za mapato ili
kuwezesha vijana wanawake na watu wenye ulemavu na mikopo hiyo iwe yenye
tija na itakayowezesha kujikwamua kiuchumi” alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
wa Wilaya ya Tanganyika Bw. Dotto Kwigema amesema kuwa pikipiki hizi
zitakuwa chachu katika utendaji wa kazi wa Maafisa maendeo ya jamii na
zitasadia kufuatilia na kuhamasisha wananchi katika kushiriki shughuli
za maendeleo na kusaidia kupambana na ukatili wa kijinsia hususan
kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Ameongeza kuwa kwa Kata tatu
ambazo Maafisa Maendeleo ya Jamii wake hawajapata pikipiki Wilaya ya
Tanganyika itatenga Bajeti kwa ajili ya kununua pikipiki hizo ili
kukamilisha kwa Kata zote kuwa na pikipiki kwa ajili ya Maafisa hao.
Naye Afisa Maendleo ya Jamii Kata
Kabungu Wilayani Tanganyika Bw. Othman ameishukuru Serikali ya Awamu ya
Tano wa kujenga mazingira wezeshi kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii hasa wa
Kata kwa kuhakikisha wanapata nyenzo za usafiri ili kuweza kuwafikia
wananchi masikini.
Pia Afisa Maendeleo ya Jamii
kutoka Kata ya Wilayani Tanganyika Bi. Rose Mfikwa amemuhakikishia
Waziri kuwa watatumia pikipiki hizo kuhamasisha jamii ya wana- Katavi na
Wanatanganyika katika kuondoka na mila zinye hitilifu za kuozesha
watoto na kupambana na ndoa na mimba za utotoni mkoani humo.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Wanawake UN Women wametoa jumla ya pikipiki 15
kwa mkoa wa Katavi ikiwa ni jitihada za kuwezesha upatikani wa usafiri
kwa lengo la kuwafikia wananchi hasa wa vijijini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...