Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar,  Riziki Pembe Juma akitoa nasaha kwa wahitimu wa  kada mbali mbali katika  Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar  University ( ZU) wakati wa mahafali 17 ya chuo  hicho huko Tunguu Wilaya ya Kati Unguja .
Baadhi ya wahitimu wa chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar University wakitunukia vyeti  wakati wa Mahafali 17 ya chuo hicho huko  Tunguu Wilaya ya Kati Unguja .
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar,  Riziki Pembe Juma akimkabidhi Cheti cha Elimu ya Master Muhitimu Khamisuu Hamid Mohamed  huko katika Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar  University  Tunguu Wilaya ya Kati Unguja .
Baadhi ya Wahitimu wa  kada mbali mbali wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Riziki Pembe Juma  ( hayupo pichani) akitoa nasaha kwa wahitimu wa  Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar  University ( ZU)wakati wa Mahafali 17 ya chuo hicho huko  Tunguu Wilaya ya Kati Unguja .

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar      
Wahitimu wa vyuo vikuuu wametakiwa kulipa mikopo waliopatiwa  na Bodi ya Mikopo Zanzibar kwa ajili ya masomo yao ili na wengine wapate fursa hiyo ya kuendeleza masomo yao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Riziki Pembe Juma wakati wa mahafali ya 17  ya kuwatunukia  vyeti  wahitimu wa fani mbali mbali katika  Chuo kikuu cha taifa  Zanzibar  University ( ZU) Tunguu Wilaya ya Kati Unguja

Amesema iwapo wahitimu hawatoweza kulipa mikopo waliopatiwa kwa wakati muwafaka,  watasababisha wengine kupata  fursa ya mikopo hiyo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa  bodi hiyo.

Amesema kuwepo kwa University Zanzibar  kumeleta maendeleo ya kiuchumi  visiwa vya Zanzibar,Tanzania na Afrika kwa ujumla na kumesaidia ongezeko kubwa la wanafunzi  katika mwaka huu kulinganisha na mwaka uliopita ambao ulitoa wahitimu  9344  katika kada tofauti 4516 wanaume na 4828 wanawake ambao wapo Serikalini na sekta binafsi.

Aidha Waziri Pembe amefahamisha kuwa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar kulikua kuna idadi ndogo ya wahitimu wa Vyuo Vikuu, ukilinganisha na hali ilioyopo hivi sasa na wahitimu wanaume waliongoza katika  kufaulu kuliko wanawake. kutokana  na mfumo dume uliokuwepo awali,baada ya kuwepo  sayansi na teknololojia wanawake wengi wanajipatia elimu kwa idadi kubwa ya ufaulu wa hali ya juu .

Nae katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Idriss Muslih Hijja amesema Zanzibar University ni chuo cha mwanzo kinachoongeza kada za masomo mbali mbali  na wanatarajia kuongeza miundombinu ya vifaa vya masoma ili kuleta maendeleo kwa wanafunzi waliopo hapo.

Hata hivyo amesema kuwa mpango uliopo kwa sasa ni kujenga jengo jipya na kutoa ofisi mbali mbali  ili kutatua tatizo  hilo na kutafuta miradi mbalimbali ya kuongeza kipato kwa wanafunzi na walimu jambo ambalo litasaidia ufanyaji kazi kwa ufanisi mkubwa

Kwa upande wa wahitimu wa Chuo hicho akiwemo Pili Sheha Khamisi kwa niaba ya wenzake wameiomba Serekali kuwapatia ajira ili waweze kulipa mkopo waliopatiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...