KAMPUNI ya.Mafuta ya Puma Tanzania ambayo ni namba moja katika biashara ya mafuta imeng’ara kwa kujinyakulia tuzo nne katika hafla ya kuwazawadia waajiri bora nchini iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ya utoaji tuzo iliandaliwa na Umoja wa Waajiri Tanzania (ATE) ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Kazi, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemeavu Jenista Mhagama.
Wakati wa kukabidhiwa tuzo hizo za ATE , Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilitangazwa mshindi katika vipengele vifuatavyo.Tuzo hizo ni Mwajiri Bora mwenye mkakati bora zaidi wa kwa kuvutia na kutunza vipaji (Best Attraction and Retention Strategies), Mwajiri Bora katika kutunza na kusimamia wafanyakazi wenye umri mkubwa (Best employer In Managing Aged workface).
Pia kampuni ya Puma Energy iliibuka mshindi wa tatu katika kipengele cha Mwajiri bora kutoka sekta binafsi pamoja na kushika nafasi ya tatu katika tuzo kuu ya mwajiri bora wa mwaka 2019 baada ya TBL na GGM.
Akizungumza baada ya kushinda tuzo hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah aliwanpongeza washindi wote pamoja na makampuni mengine mbalimbali yalioshiriki katika tuzo hizo ma kwamba mwaka huu ameshuhudia mtanange mkali baina ya kampuni jambo linaloashirikia uboereshwaji mkubwa wa mazingira ya biashara nchini.
'Lakini kubwa zaidi uboreshwaji wa sera za usimamizi wa rasilimali watu nchini.Mwaka huu 2019 Puma Energy Tanzania imesani mkataba wa hali bora mahali pa kazi ( Collective Bargaining Agreement) na chama cha wafanyakazi TUICO, mkataba huu umeboresha Sanaa hali na mazingiira ya kazi kwa wafanyakazi wa kampuni yetu.
"Kama kampuni namba moja Tanzania katika biashara ya Mfuta ni wajibu wetu kuendelea kuboresha hali za wafanyakazi wetu lakini zaidi jamii mbalimbali zinazo tuzunguka. Tutaendelea kufanya wajibu wetu kama Mwajiri makini nchini Tanzania,"amesema Dhanah.
Kuhusu kampuni hiyo, Dhanah amesema kuwa Puma Energy Tanzania ni kampuni ya mafuta iliyosajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba inamilikiwa kwa pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited.
Amefafanua kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50. Kampuni ya Puma ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.
"Majukumu makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta 94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege,amesema Dhanah.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Dominic Dhanah akiwa
ameshika tuzo mbili kati ya nne ambazo wamezipata kutoka kwa Umoja wa
Waajiri Tanzania(ATE)
Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushinda tuzo nne kati ya 10.ambazo.zimetolewa na Umoja wa Waajiri Tanzania( ATE)
Kutoka kushoto Afisa rasilimali watu Joseph Jaruma, Katibu wa chama cha wafanyakazi Derick Kajukano, Meneja rasilimali watu Loveness Hoyange, Maneja wa Vituo Vya mafuta Vanessy Chilambo, Mkurugenzi wa Puma Energy Dominic Dhanah wakifurahia Mara baada ya kushinda Tuzo katika hitomisho la usiku wa Tuzo Za kumsaka muajiri bora zilizofanyika DSM. Kampuni ya Puma ili shinda Tuzo 4
Kutoka kulia ni Meneja oparesheni wa kampuni ya Puma upande wa usafiri wa anga Benjamin Masige, Mkurugenzi Mtendaji Domnic Dhanah, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu (Afrika), wakionyesha tuzo nne walizozishinda jana katika hafla ya tuzo za Umoja wa Waajiri Tanzania (ATE).
Mgeni Rsmi katika ghafla ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na Umoja wa Waajiri Tanzania(ATE) Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Kazi, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemeavu Jenista Muhagama (kushoto)akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Dominic Dhanah(kulia) ,katikati ni Ofisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Puma Afrika Lovennes Hoyange wakijadiliana jambo wakati wa ghafla hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...