Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii-Mwanza

JUMLA ya Sh.milioni 600 zinatarajiwa kutumika katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 kwa ajili ya ukarabati wa daraja la meli katika Bandari ya Musoma ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha bandari hiyo inarejea kutoa huduma za kusafirisha mizigo na abiria.

Hayo yamesemwa leo Desemba 6, mwaka 2019 na Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa Morris Mchindiuza wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA)katika katika kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma baada ya muda mrefu kusimamishwa kwa shughuli zake kutokana na sababu mbalimbali.

"Mkakati wetu katika bandari ya Musoma ni pamoja na kuboresha miundombinu yake.Hata hivyo tayari tumeweka lengo la kuhakikisha tunakarabati daraja la reli ili kuhakikisha mizigo mingi inaptishwa katika bandari hii hasa kwa kuzingatia wafanyabishara kadaa wamekuwa wakiitumia kusafirisha mizigo ikiwemo ya pamba.

"Zamani bandari ya Musoma ilikuwa inatoa huduma zake za kuhudumia wananchi lakini baada ya kukamilika kwa barabara kati ya Musoma na Mwanza , bandari hii ikaanza kusuasua kutoa huduma na hasa ya kubeba mizigo kwani watu wengi walimua kusafirisha kwa kutumia usafiri wa barabara.

"Sababu nyingine ni mdororo wa uchumi kwa kipindi cha hapo nyuma lakini tangu Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani na kuweka mikakati thabiti ya kuboresha sekta ya bandari na miundombinu kwa ujumla, tumeamua kuiboresha miundombinu ya bandari hii kutokana na umuhimu wake,"amesema Mchindiuza .

Akifafanua zaidi sababu za kukarabari daraja la meli katika eneo hilo, amesema kuna mfanyabishara wa mpamba amekuwa akitumia bandari hiyo kusafirisha pamba yake na wakati huo huo kuna mfanyabishara mwengine ameomba kuitumia kwa kupitisha saruji.

Hata hivyo matarajio ya ya TPA ni kuona huduma katika bandari ya Musoma zinakuwa za uhakika na hiyo itafanikiwa kutokana na mikakati iliyopo sasa.TPA Kanda ya Ziwa tunataka kuona tunahudumia maelfu ya wateja na sio mteja mmoja mmoja." 
 Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa Morris Mchindiuza  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kuihuhisha bandari ya Musoma ambayo kwa siku za nyuma utoaji wa huduma zilikuwa zimedorora.
 Ni sehemu ya daraja la meli ambalo lipo katika Bandari ya Musoma mkoani Mara ambapo imeelezwa Sh.milioni 600 zitatumika kwa ajili ya kufanya ukarabati wa daraja hilo ili kuhakikisha meli za mizigo zinatoa huduma bandarini hapo.

 Mmoja ya watumishi wa Bandari ya Musoma Mjini akizungumzia umuhimu wa bandari hiyo kwa wananchi wa Mkoa wa Mara na maeneo jirani ya mkoa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...