Mmoja wa wananchi akiwa amebeba gunia la dagaa kabla ya kupakiwa katika boti katika gati la Mwigobero katika Bandari ya Musoma mkoani Mara.
Mkazi wa Musoma Mjini akiendelea kupanga magunia ya dagaa katika gati la Mwigobero lililopo katika Bandari ya Musoma mkoani Mara.
 Baadhi ya wananchi wakiwa katika Bandari ya Musoma katika gati la Mwigobero wakiwa katika boti kabla ya kuanza safari ya kutoka bandarini hapo

 Wananchi wakiwa wanaendelea na shughuli zao katika bandari ya Musoma katika gati la Mwibobero leo Desemba 6, mwaka 2019.Moja ya shughuli ambazo wananchi hao wanafanya ni kujaza samaki aina ya dagaa kabla ya kusafirishwa kuelekea maeneo mengine ya nje ya Mkoa wa Mara.

 Mmoja wa akina mama wanaofanya kazi ya kujaza dagaa katika magunia katika gati la Mwigobero katika Bandari ya Musoma mkoani Mara.
 Wananchi wakiwa katika boti na wengine wakipakia mizigo kabla ya kuanza kwa safari ya boti hiyo kutoka gati la Mwigobero.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Musoma

WATUMIAJI wa Bandari ya Musoma ambao wamekuwa wakiitumia bandari hiyo kusafirisha mizigo yao pamoja na abiria waipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Kanda ya Ziwa kutokana na juhudi zinazoendelea za kuboresha miundombinu ikiwemo ya kukamilisha ujenzi wa gati la Mwigobero.

Wakizungumza na Michuzi Globu ya Jamii mkoani Mara wakiwa katika shughuli zao za kiuchumi, baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa kujengwa kwa gati la Mwigobero kumemsha matumaini mapya ya kuimarishwa kwa huduma za usafirishaji wa mizigo midogo midogo pamoja abiria.

"Kwetu sisi ni faraja kuona gati hili ambalo limejengwa limekamilika. Tunaamini kuwa tunakokwenda hata changamoto ambazo zimekuwa zikitukabili zipata ufumbuzi wake, Serikali ya Awamu ya Tano na Mamlaka ya Bandari Tanzania wameonesha umuhimu wa kuisimamia vema sekta ya bandari,"amesema mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Wanchari ambaye anafanya shughuli za kubeba mizigo.

Kwa upande wake Shomari Masenza amesema kukamilika kwa gati la Mwigobero angalau kumeongeza usalama wa watumiaji wa ziwa Victoria katika eneo hilo huku akishauri kuendelewa kuboreshwa zaidi kwa miundombinu ili kutoa nafasi kwa wanaotumia eneo hilo kusafirisha mizigo yao kuwa salama zaidi.

Hata hivyo uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania katika Ziwa Victoria umesema umejipanga kuboresha huduma za bandari katika Ziwa hilo na miongoni mwa bandari ambazo zimepewa kipaumbele ni Bandari ya Musoma ambapo Sh.605,036,150 .00 zimetumika kujenga gati huku ikisisitiza kutarajia kutumia Sh.milioni 600 kwa ajili ya ukarabati daraja la meli.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...