Afisa wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Tabora Godfrey Comoro akitoa mafunzo ya elimu kuhusu namba ya utambulisho wa mlipa kodi TIN wafanyabiashara pamoja na wajasiliamali walioshiriki katika mafunzo ya Urasimishaji wa Biashara Mkoa wa Tabora.

 Baadhi ya wafanyabiashara pamoja na wajasiliamali walioshiriki katika mafunzo ya siku Nne ya Urasimisaji biashara kwa lengo la kuwafanya kuwa rasmi,kuweza kutunza kumbukumbu pamoja na kutambulika katika taasisi za kifedha
 Meneja wa Urasimishaji biashara kutoka Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA Harvey Kombe aazkitoa mafunzo kwa wajasiliamali na wafanyabiashara walioshiriki katika mafunzo ya Urasimishaji Mkoa wa Tabora.
Afisa Urasimishaji na uendelezaji biashara kutoka MKURABITA Zablon Makoye akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa kuweka kumbukumbu katika biashara na jinsi ya kutambulika katika taasisi za kifedha kwa wafanyabiashara na wajasiliamali wa Mkoa wa Tabora.



Tabora.

Imeelezwa kuwa sababu kubwa ya kufungwa kwa biashara nyingi hapa Nchini kunatokana na wafanyabiashara kushindwa kutofautisha matumizi ya faida na mapato ya mali binafsi na mali za biashara .

Hayo yamesemwa na Meneja wa Urasimishaji biashara kutoka Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA Harvey Kombe wakati akitoa mafunzo kwa wajasiliamali na wafanaya Biashara zaidi ya mia Mbili wa Mkoa Tabora yaliyolenga kutoa elimu juu umuhimu wa kurasimisha biashara na kuzifanya kuwa katika mfumo rasmi unaotambulika.

Kombe amesema kuwa biashara nyingi zinadumu kwa kipindi cha miaka michache na kufa kutokana na wafanyabiashara kuchanganya matumizi binafsi na matumizi kutoka katika mitaji ya biashara na hivyo kusababisha kushindwa kujiendesha.

“Wafanyabiashara wengi wa Tanzania hawatofautishi mali za biashara na mali binafsi hawajilipi mishahara na matokeo yake ni kwamba matumizi yao bianafsi wanachukua kwenye mtaji wa biashara na ndio inasababisha zikifikisha miaka miwili mitatu zinakufa kwa sababu mtaji wa biashara unatumika kinyume na kanuni za kuendesha biashara”amesema Kombe

Ameongeza kuwa ili mfanyabiashara aweze kujua faida halisi ya biashara anayoiendesha anapaswa kuweka kumbukumbu ambayo itaonesha kiasi gani kinachopatikana katika biashara yake..

“Biashara iliyo rasmi Yenyewe iwe inatunza kumbukumbu za mahesabu mfanya biashara aweze kujua faida halisi ya biashara anayooendesha lazima awe anatunza kumbukumbu bila kuwa na kumbukumbu za biashara sio rahisi kujua anapata faida kiasi gani na anapata hasara kiasi gani.”Kombe

Akitoa elimu kuhusu namba ya utambulisho wa mlipa kodi TIN afisa wa TRA mkoa wa Tabora Godfrey Comoro amesema kuwa kuna aina mbili za TIN ambazo mwananchi anaweza kuwa nayo lakini mfanyabiashara lazima awe na TIN inayomtambulisha kwa nafasi yake.

“Tin ya kwanza ni kwa ajili ya shughuli zisizo za kibiashara kwa mfano mtu anataka leseni ya udereva kwa ajili ya kutumia vyombo vya moto au anataka kununua gari nje ya nchi au amenunua hapa nchini anataka kusafirisha na TIN ya pili ni kwa ajili ya kupata leseni ya biashara ambapo mfanyabiashara ataweza kufanya biashara mbalimbali ambazo zinatambulika rasmi.

Zaidi ya wafanyabiashara na wajasiliamali elfu moja wa Manispaa ya Tabora wameshiriki katika mafunzo hayo ambapo taasisi mbalimbali za kifedha zimetoa elimu ya utoaji wa mikopo pamoja na njia sahihi za kurejesha kwa wakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...