Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imetangaza idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari kwa kidato cha kwanza mwaka 2020 kuwa ni 700, 138 sawa na asilimia 92.27.

Katika idadi hiyo mikoa 13 ya Tanzania bara ikiwemo Dodoma, Shinyanga, Geita, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Morogoro, Mtwara, Njombe, Ruvuma, Singida na Mwanza imeweza kuchagua wanafunzi wote waliofaulu mitihani yao ya Darasa la saba na kujiunga na kidato cha kwanza.

Akitangaza mchanganuo huo jijini Dodoma leo mbele ya wandishi wa habari, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mhe Selemani Jafo amesema kati ya wanafunzi hao waliochaguliwa wavulana ni 335513 sawa na asilimia 13 wakati wasichana wakiwa ni 365525 sawa na asilimia 52.14.

Waziri Jafo ameongeza kuwa kati ya wanafunzi 1161 waliochaguliwa kati ya waliofaulu ni wale wenye ulemavu ambao ni sawa na asilimia 0.41.

" Wanafunzi 3145 sawa na asilimia 0.41 ya waliofaulu wamechaguliwa kujiunga na bweni,ambapo wanafunzi 970 watajiunga  na shule ya vipaji maalum,huku 1095 watajiunga na shule za ufundi na 1080 watajiunga na shule za bweni za kawaida.

Hata hivyo,wanafunzi laki 6 na 97 elfu mia 893 sawa na asilimia 99.59 wakiwemo wavulana laki 3 na 61 elfu 866 na wasichana laki 3 95 elfu mia 6 92 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa katika kata mbalimbali nchini," Amesema Waziri Jafo.

Mhe Jafo amesema kutokana na baadhi ya maeneo nchini kuwa na changamoto ya uhaba wa madarasa imechangia wanafunzi 58,699 sawa na asilimia 7.73 wakiwemo wavulana 28,567 na wasichana 30,132 kukosa nafasi za kujiunga na masomo yao ya kidato cha kwanza.

Ameitaja Mikoa yenye uhaba wa vyumba vya madarasa ni pamoja na Arusha, Dar es Salaam, Iringa, Kigoma, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Pwani, Simiyu, Rukwa, Songwe na Tanga ambapo pia amewapongeza Wabunge kwenye baadhi ya maeneo ambao wamechangia kuweza kupatikana kwa vyumba vya madarasa.

Amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kote nchini kuhakikisha wanafanya maandalizi ya kuwapokea wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza huku pia akiwaagiza viongozi wa maeneo yenye changamoto ya madarasa kumaliza changamoto hiyo ili wale ambao hawajapata nafasi waweze kujiunga na wenzao ifikapo Machi 2020.

" Kumekuepo na mkanganyiko wa michango gani ambayo wazazi wazazi wanapaswa kutoa pindi watoto wao wanapojiunga na kidato cha kwanza, niwatake wazazi kugharamia mahitaji binafsi ya watoto wao ikiwemo madaftari, sare za shule na wasitoe michango yoyote bila kuwa na ridhaa ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya wa eneo husika," Amesema Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dodoma wakati akitangaza uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 Tanzania bara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...