Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya Bw. Bernard Konga akiongea na waandishi wa habari leo
Jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya mfuko huo katika kipindi cha miaka
minne ya Serikali ya Awamu ya Tano (4), Kushoto ni Afisa Habari Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Catherine Sungura
na Kulia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Angela
Mziray

Waandishi wa
Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Bw. Bernard Konga wakati akiongelea kuhusu mafanikio ya mfuko huo katika
kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano
PICHA NA IDARA YA HABARI- MAELEZO
…………….
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) umetajwa kuwezesha mageuzi yenye tija katika sekta ya afya katika
kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano .
Akizungumza waandishi wa habari
leo, Desemba 12, 2019 Jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya mfuko huo,
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Bw. Bernard Konga amesema kuwa baadhi ya
Hospitali zilizonufaika ni Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bugando, KCMC,
MOI, Ocean Road,na Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa kuwezeshwa kupata
vifaa kama MRI, CT SCAN, uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kuzalisha
maji ya dripu, gesi na ujenzi wa majengo.
‘’ NHIF imetoa fedha kuwezesha
uwekezaji wa awamu ya pili katika Hospitali ya Benjamin Mkapa na
ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa kuwezesha huduma za kibingwa kama
upandikizaji figo, ambapo shilingi Bilioni 32.10 zimetolewa kwa ajili
ya ujenzi na Bilioni 43.12 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa katika
Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma ’’ Alisisitiza Konga
Akifafanua amesema kuwa uwekezaji
wa majengo pacha ya MOI umesaidia kuongeza uwezo wa kulaza wagonjwa na
kuboresha huduma za Kibingwa katika Taasisi hiyo, majengo mengine
yamejengwa kwa uwekezaji wa NHIF katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda
Mbeya, Hospitali ya Rufaa Dodoma, Hospitali ya Rufaa Bugando na KCMC.
‘’Wanachama wa NHIF wanapata
huduma katika vituo 7,606 nchi nzima vikiwemo vya Serikali na Binafsi
kwa ngazi zote ikilinganishwa na vituo 6,185 vya mwaka 2014/2015
,Ongezeko hili ni sawa na vituo 1,421 kwa kipindi cha miaka
minne’’. Alisistiza Konga
Katika kipindi cha miaka minne,
NHIF imelipa jumla ya shilingi trilioni 1,283,109,701,067 kwa vituo
vyote vinavyohudumia wanachama wake nchini wakati mwaka 2018/2019 Mfuko
umelipa kiasi cha Shilingi Bilioni 444.1 ambayo ni ongezeko la asilimia
64 ikilinganishwa na malipo yaliyofanyika mwaka 2014/2015 ya shilingi
bilioni 157.9
Akizungumzia utekelezaji wa mradi
wa Tumaini la Mama ulilenga kuwapatia wanawake wajawazito Bw. Konga
amesema kuwa mradi huo umetekeelzwa kupitia NHIF na umewanufaisha jumla
ya akina mama milioni 1,044,000.
Katika kipindi cha miaka minne
mradi huu umewanufaisha akina mama 796,404 sawa na ongezeko la la
asilimia 76 kutoka wanufaika 247,596 wa mwaka 2014/2015 mradi huo
umesaidia kupunguza vifo vya uzazi na umewezesha wakinamama
kujifungulia Hospitali.
Serikali kupitia Wizara ya Fedha
na NHIF imesaini mkataba wa awamu ya tatu na KfW wenye thamani ya EURO
milioni 13 sawa na Shilingi Bilioni 32.7 kuwezesha utekelezaji wa mradi
huo utakamilika mwaka 2020.
NHIF imethibitishwa kwa utoaji
wa huduma bora kwa viwango vya kimataifa na kukabidhiwa cheti cha
ubora (ISO 9001:2015) mwaka 2018, ndani ya kipindi cha miaka minne ya
Awamu ya Tano, mfuko umeimarisha mawasiliano na wanachama na wadau wake
kwa kuanzisha Kituo cha Huduma kwa Wateja.
Mfuko unahudumia wanachama 966,792
sawa na wanufaika 4,025,693 ikilinganishwa na idadi ya wanufaika
3,237,434k kwa mwaka 2014/15 sawa na ongezeko la asilimia 20.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...