Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii-Mwanza 
SERIKALI ya Awamu ya Tano imeamua!Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Serikali kutenga Sh.bilioni 152 kwa ajili ya kutekeleza miradi minne ikiwemo ya kukarabati meli kubwa, kujenga meli mpya pamoja na chelezo ya kisasa. 

Akizungumza leo Desemba 7,mwaka 2019 jijini Mwanza, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Eric Hamissi amesema chini ya Rais Dk.John Magufuli ambaye amekuwa na maono ya kuifikisha Tanzania mbali kiuchumi na kimaendeleo, kuna miradi mikubwa minne inayoendelea katika kuboresha huduma za meli nchini. 

"Tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha sekta ya meli inakuwa bora na imara.Hivyo kwa mara ya kwanza Serikali ndani ya kipindi kifupi imetenga Sh.bilioni 152 kwa ajili ya kutekeleza miradi minne ya kujenga meli mpya na kukarabati meli nyingine za zamani,"amesema. 

Amefafanua zaidi amesema Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Eric Hamissi kwa sasa wana meli 14 na boti moja ambazo zipo katika Maziwa Makuu ya Victoria, Nyasa na Tanganyika.Amezitaja meli hizo ni Mv.Wimbi, Mv. Sangara, Mv. Umoja na Mv. Clarias. 

"Tuna meli nne ambazo zinafanyakazi kwa sasa ambazo ni Mv. Wimbi, Mv. Sangara, Mv. Umoja na Mv. Clarias. Pia tuna wakandarasi ambao sasa wanaendelea na kazi ikiwamo ujenzi wa chelezo ambapo Kampuni ya Six Engine na Saekyung Construction zinaendelea na kazi hiyo ambayo kwa sasa imefika zaidi ya asilimia 68. 

"Ujenzi meli mpya ya Mv. Mwanza Hapa Kazi Tu, inafanywa na Kampuni ya Gas Entec na Kangnam Corporation za nchini Korea Kusini ambapo wanafanya kazi hii kwa kushirikiana na Suma JKT na ukarabati wa meli za zamani kazi hii inafanywa na Kampuni ya KTM ambayo inakarabati meli mbili za Mv. Victoria na Mv. Butiama," amesisitiza Hamissi. 

Wakati huo huo amesema pindi meli ya Mv. Mwanza itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200, magari madogo 20 na malori makubwa matatu. "Meli hiyo itakuwa na uzito wa tani 3,500 huku chelezo ya kisasa inayojengwa ikiwa na uwezo wa kubeba tani 4,000.Ujenzi wa chelezo hiyo ya kisasa ni sehemu ya miradi ya kuboresha huduma za meli." 

Kuhusu Kampuni hiyo amesema awali hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) mwaka 1997.Hata hivyo miaka michache baadae Serikali ikaingia katika mchakato wa kutaka kulibinafsisha Shirika. 

Hata hivyo amesema kuwa Kampuni hiyo kwa nyakati tofauti imepita katika kipindi kigumu na ilipofika mwaka 2015, Rais Magufuli alipokuwa akiomba ridhaa ya Watanzania aliahidi kufufua meli na kuleta meli mpya katika maziwa yote makuu nchini. "Hivyo ili kuhakikisha ahadi hiyo na nyingine zinatekelezwa Serikali ilimua kutoa jukumu hilo kwa kampuni yetu na sasa tumesimama na tunaendelea kutoa huduma".
 Meli ya MV.Victoria ikiwa katika chelezo kwa ajili ya kukarabatiwa ikiwa ni mkakati wa Serikali kuboresha usafiri wa meli katika Ziwa Victoria.
 Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Eric Hamissi akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mikakati mbalimbali inayoendelea katika kuimarisha usafiri wa meli nchini. 
 Meli ya MV.Victoria ikiendelea kukarabatiwa  ambapo inatarajia kukamilika mwakani ili kuanza kutoa huduma.


 Ujenzi wa eneo la chelezo inayojengwa katika eneo la Bandari ya Ziwa Victoria Mjini Mwanza ukiendelea. Inaelezwa Rais Dk.John Magufuli kesho Desemba 8,2019 anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo.
Baadhi ya mafundi wanaotengeneza meli ya MV.Victoria wakiendelea na majukumu yao.
Picha zote na Said Mwishehe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...