Mtume Paul Toritseju kutoka Nigeria (kushoto) Mchungaji  Dkt.  Sako Mayrick wakiongoza maombi katika semina ya uponyaji inayoendelea leo  Success Chapel Jengo la Ushirika Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Mtume Paul Toritseju kutoka Nigeria, akimuombea Anastazia Raphael.
 Mtume Paul Toritseju kutoka Nigeria, akimuombea Jackson Juma.
 Maombi yakiendelea.
 Mtume Paul Toritseju kutoka Nigeria, akimuombea mtoto.
Maombi yakiendelea.

Na Dotto Mwaibale
 VIJANA mbalimbali wameendelea kujitojeza kwa wingi katika Semina ya uponyaji inayofanyika Success Chapel Jengo la Ushirika Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Semina hiyo ya siku tatu ambayo itafikia tamati leo,  inaongozwa na  Mtume Paul Toritseju kutoka Nigeria kwa kushirikiana na Mchungaji mwenyeji  Dkt.  Sako Mayrick.
Akizungumzia kuhusu semina hiyo Dkt.Mayrick alisema ni muhimu sana kwa vijana kwani inamafundisho mengi ya uponyaji.
Alisema  katika senina hiyo washiriki wanampokea Yesu Kristo pamoja na uponyaji wa magonjwa mbalimbali, amani ya moyo, ushindi wa dhambi, ushirikina, ulozi, nuksi, mikosi na laana katika maisha.
"Katika semina hiyo unapokea ulinzi wa Mungu katika maisha yako" alisema Mchungaji Mayrick.
Mchungaji Mayrick alitumia nafasi hiyo kuwaalika watu mbalimbali kufika katika siku ya mwisho ya semina  na kuwa kwa kesho Jumamosi kutakuwa na semina ya ndoa ambayo itaanza saa 2:30 asubuhi hadi saa 8 mchana.
Alisema katika semina hiyo mada mbalimbali zitatolewa na wachungaji wenye uzoefu mkubwa hivyo watu wote wanakaribishwa na kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu namba  0758531973.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...