Hafsa Omar-Kigoma
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Desemba 20,2019 amefungua kiwanda cha Nguzo cha Qwihaya, kilichopo katika Mtaa wa Kasanga, Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, mara baada ya ufunguzi wa kiwanda hicho Dkt. Kalemani alieleza kuwa Serikali ilikuwa inapata gharama kubwa kutoa Nguzo katika Mikoa mengine kuzifikisha Mkoani humo kabla ya kiwanda hicho kujengwa Mkoani humo.
Alisema, maeneo ambayo yapo karibu na kiwanda hicho yatafikiwa na umeme kwa haraka kwasababu hakutakuwa na sababu ya ucheleweshaji wa kupeleka umeme katika maeneo hayo ambayo, kiwanda cha nguzo kipo karibu.
Aliongeza kuwa, Serikali haitakubali  kuona ucheleweshwaji wa usambazaji umeme vijijini, kupitia TANESCO au  Wakandarasi, kwasababu ya uwepo wa kiwanda hicho Mkoani humo umewarahisishia kazi na  bei ya nguzo itashuka ikilinganishwa na bei ya Nguzo ambazo zinatoka katika Mikoa ya Njombe na Iringa.
“ Maelekezo yangu kwa TANESCO ni kuanza kuzichukua nguzo hizi kwa njia ya ushindani hakuna tena sababu ya kusema nguzo hakuna na nataka kazi zimalizike ndani ya muda kwasabau vitendea kazi vipo na pesa ipo” alisema.
Alifafanua kuwa, mahitaji ya nguzo kwa sasa nchini ni milioni moja na nusu kwa mwaka lakini wazalishaji nchini wanauwezo wa kuzalisha zaidi ya  nguzo milioni tatu ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo mahitaji ya nguzo yalikuwa milioni moja na nusu lakini nguzo zilizokuwa zinapatikana nchini ni laki nne tu, ambapo nguzo nyingi zilikuwa zinatoka Nchi za nje lakini kwa uwepo wa viwanda nchini imesaidia sana upatikanaji wa nguzo kwa wingi.
Alieleza kuwa, kwa kipindi cha miaka minne viwanda vya nguzo tisa vimejengwa nchini, mara baada ya Serikali kupiga marufuku ya ununuaji nguzo kutoka nchi za nje ambao ulikuwa unachelewesha usambazaji wa umeme nchini .
Aidha, alimpongeza muwekezaji wa kiwanda hicho, kwa kujitolea  kujenga kiwanda kwenye eneo hilo pamoja na kumiliki viwanda vyengine Mkoani Njombe na Iringa na kuamua kuwekeza katika maeneo mengine ya nchini.
Kwa kuona umuhimu wa Viwanda hivyo, Waziri Kalemani ametoa wito kwa wawekezaji wengine wajitokeze kujenga viwanda vya Nguzo, katika Mikoa mengine nje ya Mkoa wa Iringa na Njombe ili kutimiza azma ya Rais ya Tanzania ya Viwanda.
Awali, Kaimu  Mkurugenzi wa kiwanda hicho Beruto Kaboda ameleza kuwa kiwanda chao kimeamua kimeitikia wito wa Rais, wa Tanzania ya Viwanda kwa vitendo kwa kuchukua hatua ya kujenga kiwanda hicho  chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya nguzo laki moja kwa mwaka.
 Vile vile, alieleza kuwa kwasasa soko lao kubwa lipo hapa nchini na mteja wako mkubwa ni Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) ambapo kipindi hiki cha utekelezaji wa mradi wa  REA awamu ya tatu soko la nguzo limekuwa kubwa na kuwalazimu kufanya kazi kwa masaa 24.
Pia alitoa shukrani zake kwa Waziri wa Nishati Dr Medard Kalemani na Naibu Waziri Subira Mgalu kwa kuwasimamia wazalishaji wa nguzo nchini na kutoa miongozo ambayo inawapa hamasa ya kufanya kwa bidii na kuhakikisha  wanazalisha nguzo bora na zinawafikia wananchi wa vijiji kwa haraka zaidi.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( mwenye shati la bluu) akiwasili kwenye ufunguzi wa kiwanda cha Nguzo cha Qwihaya kilichopo wilayani Kasulu.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, akipata maelekezo kuhusu kiwanda cha Qwihaya kutoka kwa mmoja wa mfanyakazi wa kiwanda hicho.
Nguzo za umeme zinazozalishwa na kiwanda cha Qwihaya zikiwa tayari kwaajili ya matumizi.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kiwanda cha nguzo cha Qwihaya.

Waziri wa Nishati, Dkt Kalemani akimpongeza Leonard Mahenda ambae ndio mmiliki wa kiwanda cha Qwihaya mara baada ya kukata utepe.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...