JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuujulisha umma kuwa huduma ya Usajili na Utambuzi wa Watu, na Ugawaji wa Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) itatolewa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam kuanzia leo Jumatatu tarehe 23 hadi 31/12/2019 kuanzia saa 02:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni.
Huduma ya utoaji wa Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) inatolewa kwa wakaazi wa mikoa yote.
Usajili (kupigwa picha, kuweka saini ya kielektroniki na kuchukuliwa alama za vidole) inatolewa kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam tu.
Waakazi kutoka mikoa mingine wanaohitaji huduma ya Usajili watatakiwa kufika katika ofisi za Usajili za NIDA katika wilaya wanakoishi.

Sherehekea Krisimasi na Mwaka Mpya ukiwa na Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN) ili Usajili Laini ya Simu na kupata huduma nyingine.
Karibu tukuhudumie.
Imetolewa na;
Thomas W. Nyakabengwe
Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati
22/12/2019
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...