Mara kadhaa tumekua tukiona Rais Magufuli akiwaapisha mabalozi wateule ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Katika miaka mitano ya uongozi wake, Rais Magufuli ameteua jumla ya mabalozi 42 na Mabalozi wadogo watatu hivyo kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya wawakilishi 45 kati ya mataifa 195 yanayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Kwa wale tunaojua hesabu za kugawanya, tutagawa 195 ÷45 na kupata wastani kuwa Balozi mmoja anaziwakilisha jumla ya nchi 4 jambo linaloungwa mkono na wadau wa Diplomasia na Maendeleo. Idadi hiyo haijajumuisha Mabalozi wa Heshima waliopo sehemu mbalimbali wanaoiwakilisha nchi yetu nje.

Idadi hiyo inatokana na kuongeza jumla ya mabalozi nane katika nchi ambazo hapo awali hazikua na uwakilishi kutoka Tanzania. Mataifa hayo ni: Cuba, Korea Kusini, Israel, Qatat, Sudan, Algeria, Namibia, na Uturuki.

Mabalozi hao wameteuliwa kimkakati kabisa kwa kuzingatia manufaa watakayoyapata watanzania katika mataifa hayo. Mfano: mwaka 2019 vijana 100 wa kitanzania walikwenda Israel kujifunza kilimo chenye tija huku Tanzania ikipokea maelfu ya watalii kutoka kwenye taifa hilo la Mashariki ya Kati.

Pia, Mabalozi hao wamekua Wagunduzi wa fursa za masomo, biashara, na nyenginezo zinazopatikana kutoka kwenye mataifa ya nje.

Mungu Ibariki Afrika! Mungu Ibariki Tanzania! Mungu mbariki Rais Wetu Mh.Dr. John Pombe Magufuli. Ameeen!!

Patrick Joseph Paul
Diaspora- Uturuki
Januari 29, 2020

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...