Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, amepokea mapendekezo ya Ilani ya mwaka 2020 – 2025 kutoka kwa Jumuiya ya Walemavu Nchini.Mapendekezo hayo yametolewa kwa wajumbe na wananchi wote wenye ulemavu kutoka kanda tisa nchini
Makabidhiano hayo yamefanyika jioni ya leo tarehe 30 Januari, 2020 Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma.
Katika makabidhiano hayo, wajumbe wa Jumuiya hiyo wameishukuru na kuipongeza CCM na Serikali yake, inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, kwa kuwajali na kuweka sera rafiki na wezeshi kiuchumi, kijamii na siasa ikiwa ni pamoja na kuwazingatia katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Jumuiya hiyo imeongozwa na Mwenyekiti Ndg. Peter Sarungi akiwa na viongozi na wajumbe mbalimbali.Huu ni muendelezo wa CCM kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu kupokea mapendekezo mbalimbali kuelekea kuandika Ilani mpya Jumuishi ya Uchaguzi Mkuu kwa Mwaka 2020 – 2025, kutoka kwenye Taasisi, mashirika, vyama vya siasa na vya kijamii nchini, makundi ya wasomi na watu binafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...