Mgeni Rasmi Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta, akizungumza jambo kwa wageni waalikwa katika Hafla ya uzinduzi wa Duka la vifaa la JOTUN lililopo Masaki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kampuni za WELLWORTH ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni  ya JOTUN Tanzania, Zulfikar Ismail akizungumza akitoa shukrani kwa wageni waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa Duka la vifaa vya nyumbani la JOTUN eneo la Masaki jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen ambaye pia alikuwa Mmoja wa wageni waliohudhuria uzinduzi wa Duka la vifaa vya nyumbani la JOTUN akizungumza jambo kwenye Uzinduzi huo.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta alipokuwa anazungumza kwenye uzinduzi wa Duka la vifaa vya nyumbani la JOTUN eneo la Masaki jijini Dar es Salaam.
 Mgeni Rasmi Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni hiyo pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen wakati wa uzinduzi wa Duka la vifaa vya nyumbani la JOTUN eneo la Masaki jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Duka la vifaa vya nyumbani la JOTUN wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa duka hilo lililopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Na Yassir Simba, Globu ya jamii
Kampuni ya Jotun ikishirikiana na Hardware Afrika imezindua rasmi tawi lake jipya Masaki jijini Dar es Salaam jana tarehe 30 mwezi Januari 2020. Kampuni hiyo kutoka nchini Norway inayojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za ujenzi ikiwemo rangi imezindua tawi hili jipya visiwani na Zanzibar na jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari mgeni rasmi katika hafla hiyo Meya wa halmshauri ya wilaya ya Kinondoni, Mh.Benjamini Sitta amesema uzinduzi wa kampuni hiyo utaambatana na kutatua changamoto za bidhaa za ujenzi ikiwemo rangi na kuacha kutegemea kampuni mmoja katika upatikanaji wa bidhaa hiyo ambayo pia itatatua changamoto za upatikanaji wa bidhaa hizo za ujenzi kutokana na miradi mbalimbali ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Naye balozi wa Norway nchini Tanzania Elizabeth Yacobsen amsemema ni matumaini yake kampuni hiyo itasaidia katika ukuaji wa uchumi wa viwanda katika nchi ya Tanzania ikiwemo na uzalishaji wa bidhaa bora katika soko la Tanzania.

Aidha Mkurugenzi wa Kampuni za WELLWORTH ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni  ya JOTUN Tanzania Zulfikar Ismail amesema tawi hilo ni la tatu barani Afrika ukijumuisha na nchi za Afrika Kusini pamoja na Kenya. Pia meneja huyo amesema mikakati yap ni pamoja na kufungua matawi nchi nzima sambamba na ujenzi wa kiwanda nchini Tanzania. Akiongezea meneja huyo amedai watasaidia pia katika uzalishaji wa ajira kwa vijana nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...