Imeelezwa kuwa elimu ya sheria za
soka ikitolewa kwa wadau wa mpira ikiwemo mashabiki zitaondoa
mkanganyiko na kuwaweka huru marefarii wanaochezesha mpira wa miguu
nchini kwa kuwa wadau hao watakuwa na uelewa wa sheria hizo.
Kauli
hiyo imetolewa na Makamu mwenyekiti wa shirikisho la soka mkoani Arusha
Soud Abdi kwenye kikao cha wadau wa Michezo hususani vyama vya michezo
na Waziri wa habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Alisema
kuwa sheria za soka zinabadilika kila uchwao na wengi wa wadau hawajui
sheria hivyo timu zinazoshiriki ligi ziwe zinafundishwa sheria hizo ili
kuwawezesha wachezaji kutofanya makosa ambayo yanaweza kuepukika na
kuondoa mining'ono ambayo mwisho wa siku lawama nyingi huwaangukia
marefarii.
Alimuomba
Mh.waziri kukaa na shirikisho la soka kuona namna nzuri ya kuandaa
kipindi cha elimu ya sheria za mpira wa miguu kwenye runinga ya taifa
kwa kuwa wadau wakijua sheria hizo kutaondoa malalamiko na marefarii
watapata ahuweni pia vyama vya soka navyo vitaondokana na dhama ya
upendeleo wa timu fulani kutoka kwa timu zinazoshiriki ligi husika.
"Elimu
ya sheria ndio jawabu la kuondoa mikanganyiko kwenye mchezo wetu pendwa
wa mpira wa miguu kwa hii imewafanya wachezaji wetu kukosa timu ulaya
kwa kutojua sheria za mpira tuanze kutoa elimu hii kwenye ligi zetu
kuanzia ngazi zote kwa timu shiriki ili kuondokana na ombwe la
malalamiko" alisisitiza Abdi
Kwa
upande wake waziri Dkt.Mwakyembe aliahidi kukaa na shirikisho la mpira
nchini TFF kuona ni jinsi gani sheria zitafundishwa kwenye soka na pia
kuahidi wadau hao wa Michezo mkoani Arusha kuanzisha kipindi cha sheria
za soka kwenye runinga ya taifa huku akisifu kipindi cha kipenga kwa
kupata umaarufu na kuwafanya wadau kujua sheria.
Alisema
kuwa sheria za mpira wa miguu zinakuwa na mabadiliko tofauti na zamani
hivyo Kuna umuhimu kwa wadau kusijua sheria hizo ili kuendana na
mabadiliko hayo sanjari na kutoa elimu hiyo kwa wachezaji wetu kuache
kucheza kimazoea.
"Nimekuwa
kwenye msongo wa mawazo Sana kwa kuwa wengi wetu mmekuwa mkiandaa timu
kizimamoto kushiriki Michezo nje ya nchi jambo hili sio sahihi Sana
anzeni mchakato mapema andikeni maandiko mapema na leteni Ofisini kwangu
acheni kuendesha Michezo bila maandiko serikali ya Dkt.Magufuli
inapenda uwazi kwa kuwa naye napenda Sana Sanaa"alisema Mwekymbe.
Aliwashukuru
wanamichezo hususani vyama kwa kuwa wakweli na kutoa maoni yao ili
kuboresha Michezo hususani mashuleni na kuahidi kukaa na wizara ya elimu
kuona mtaala wa Michezo unafanyiwa kazi kwa kuwa Michezo ni ajira kubwa
Sana kwenye dunia ya Sasa.
"Hapo
awali tulifuta Michezo mashuleni tujikite kuzalisha wahandisi,madaktari
lakini bila Michezo yote ni kazi bure ndio maana tukarudisha Michezo
mashuleni yaende sambamba na masomo mengine kwa lengo la kuongeza akili
za wanafunzi hivyo ntakaa na wenzangu kuona tunaandaaje shule moja kwa
kila mkoa badala ya kuwa na utitiri wa shule za Michezo"
Suala
la kuwa na wataalamu wenye uzoefu na Michezo hususani kwenye chuo cha
Michezo Malya alisema amegundua jambo hivyo Sasa kuona umuhimu wake ili
kuboresha taaluma ya Michezo kwa kuwa na wakufunzi wenye taaluma za
Michezo kusaidia kulipeleka taifa kuwa washindani kwenye Michezo kwa
siku za usoni.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...