Na Khadija seif, Michuzi Tv

KWENYE tano bora ya wasanii wanaopeperusha bendera ya  Tanzania kwenye Muziki wa bongofleva huwezi kumuacha kumtaja msanii Rajab Harmonize.

 Harmonize alipokua akifanya mahojiano na kituo cha redio nchini amesema kwa mwaka huu anatarajia kufanya show yake katika ukumbi wa 02 arena uliopo nchini uingereza huku akiweka wazi kuwa malipo tayari yameshafanyika yeye kufanya show hiyo juni mwaka huu.

"Natumaini nitaweka historia ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika mashariki kufanya show katika ukumbi huo mkubwa wa burudani,"

Aidha, harmonize amefafanua kuwa alipokua uwanja wa vila pack kwenye mechi ya leister city dhidi ya Aston Villa alishuhudia shangwe na vifijo pale mchezaji kutoka nchini Tanzania Mbwana Samata alipoingia uwanjani kwa mara ya kwanza mara baada ya kusajiliwa na klabu ya aston Villa.

"Juzi nilivokua uwanjani nilithibitisha hilo kwani ndio mara yake ya kwanza kuingia dimbani kupitia timu ya Aston Villa tangu asajiliwe  lakini bado mashabiki walikua wakipiga yowe na wakitaja jina lake wakiwa na imani nae jambo kama hilo linatia sana hamasa sana kwake na kitaifa pia kuona hatuangushi hasa kwenye sekta ya michezo na kuipeperusha bendera ya Tanzania,"
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...