Na.Khadija seif, Michuzi Tv
WABUNIFU
washauriwa kutengeneza mavazi yanayoendana na mazingira halisi ili
kuweza kupata vitu vya kiasili na kutangaza utalii zaidi.
Akizungumza
na Michuzi Tv mbunifu mkongwe Ally Remtullah ambae siku chache
amefungua duka lake la mavazi akishirikiana na Kampuni ya high_ flyge
ambao walisaini mkataba wa kuuza nguo za aina ya kitenge ya nchini
china.
"Wabunifu wengi
wamekua wakitengeneza nguo ambazo zinatumia malighafi za nchi za wenzetu
lakini kwa upande wangu nimeamua kujikita kwenye vitenge na kanga kwani
hazibagui mtu jinsia watu wote hupendeza,"
Hata hivyo Remtullah ameeleza kuwa yupo tayari kusupport wabunifu chipukizi na kuwatafutia masoko nje na ndani ya nchi.
"Nawakaribisha wabunifu chipukizi kuleta bidhaa zao kwenye duka langu lililopo Msasani barabara ya chole,"
Pia
ametoa shukrani za dhati kwa wadau na viongozi wanaoendelea kumpa moyo
na hata wale wanaounga mkono sekta ya ubunifu wa mavazi hasa vazi la
kitenge huku akifafanua kuwa anawaheshimu na kupenda kazi za wabunifu
wengine Kama Martin kadinda, Khadija mwanamboka pamoja na Mustafa
hassanali.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...