Toleo jipya la simu CAMON 12 Pro ya hivi karibuni imewekewa  kitufe cha Msaidizi wa Google (Google assistant) ambacho kinaruhusu watumiaji kufanya mambo mengi zaidi kwenye mfumo wa Google.
Kampuni kinara ya Kimataifa ya simu za rununu ya TECNO yenye simujanja yake  ya  Camon 12 Pro ya hivi karibuni, inayowezeshwa na mfumo wa uendeshaji wa Pie ya Google (Google’s Android 9 Pie operating system), imeweka kitufe cha Msaidizi wa Google (Google assistant) kwenye CAMON 12 Pro katika mkutano wa maonesho ya teknolojia ya mwaka 2020 Januari hii.
TECNO imejiunga na kuwa mshirika  wa Google kuleta mfumo mpya wa uendeshaji kwa wateja wake. Wakati Google inafanya maboresho ya mfumo endeshi (Android) kwaajili ya kuleta ufanisi madhubuti kwenye vifaa janja vipya vya kisasa, TECNO ilizindua simu mpya ya kisasa ya CAMON 12 Pro kwa kuweka Kitufe cha Google assistant  ambayo ilioneshwa kwenye kibanda cha Google katika mkutano wa maonesho ya teknolojia 2020 ili kusaidia watumiaji kufanya mambo kwa haraka zaidi na kupangilia vitu muhimu kwenye ratiba ambavyo vinavyoweza kufanyika baadaye.
Google ikionesha Simujanja zenye kitufe cha Google Assistant kwenye banda lake katika mkutano wa maonesho ya teknolojia 2020.
TECNO CAMON 12 PRO yenye Kitufe cha Google Assistant kama ilivyooneshwa kwenye kibanda cha Google.
&TECNO inawasisitiza watumiaji wake kujihusisha kikamilifu na matumizi ya vifaa vyake na programu za ndani,& alisema Stephen HA, rais wa TRANSSION na Mkurugenzi Mtendaji wa TECNO &Tunafurahi kuanza ushirikiano huu na Google.&

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...