Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) Mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Diallo (mbele) akishuka kutoka kwenye
kivuko cha MV. Ilemela mara baada ya kukikagua kivuko hicho katika eneo
la yadi ya Songoro wakati kikisubiri kuanza kufanyiwa majaribio. Kivuko
cha MV. Ilemela kimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7 na kina
na uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100.

Baadhi ya wakazi wa maeneo ya
Kayenze wakiwa ndani ya kivuko cha MV. Ilemela wakati wa tukio la
kukifanyia majaribio. Kivuko hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma hivi
karibuni kati ya maeneo ya Kayenze na visiwa vya Bezi. MV. Ilemela
imejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7 na ina na uwezo wa kubeba
abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100.

Mbunge wa Ilemela ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina
Mabula katikati akiwapungia mkono wakazi wa Kayenze (hawapo pichani)
wakati akishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. Ilemela mara baada ya
kuwasili eneo la Kayenze wakati kikifanyiwa majaribio. Kivuko hicho
kimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7 na kina na uwezo wa
kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100.

Mamia ya wakazi wa maeneo ya
Kayenze wanaonekana wakiwa mbele ya kivuko hicho wakisikiliza hotuba
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika tukio la majaribio ya kivuko cha
MV. Ilemela lililofanyika katika eneo la Kayenze.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle akizungumza na wananchi wa
Kayenze ambapo alitoa taarifa fupi ya ujenzi wa kivuko hicho wakati wa
tukio la majaribio ya kivuko cha MV. Ilemela lililofanyika katika eneo
la Kayenze. Kushoto ni Mbunge wa Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula.

Mbunge wa Ilemela ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina
Mabula akizungumza na wakazi wa Kayenze (hawapo pichani) wakati wa tukio
la majaribio ya kivuko cha MV. Ilemela lililofanyika katika eneo la
Kayenze.
PICHA ZOTE NA TEMESA (MWANZA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...