Dar es Salaam. Uongozi wa klabu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC) umeingia mkataba wa mwaka mmoja na nusu (miezi 18) na kocha Haruna Harerimana baada ya kukidhi vigezo tulivyoweka.

Harerimana anachukua nafasi ya kocha Jackson Mayanja kutoka Uganda ambaye mkataba wake ulisitishwa kutokana na timu kutokuwa na mwenendo mzuri katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya Kimataifa.

Harerimana amepitishwa na Bodi ya timu ambayo ilipitia maombi mengi ya makocha wa ndani na nje ya nchi.

Zoezi la kutafuta kocha halikuwa rahisi kutokana na ujuzi na uzoefu wa makocha waliomba kuchukua nafasi ya Mayanja ambapo baada ya kuondoka, nafasi hiyo ilikuwa chini ya kaimu kocha mkuu, Hamadi Ally.

Kocha Harerimana ametambulishwa kwa wachezaji na tayari ameanza kazi ya kuinoa timu ya KMC kwa ajili ya mashindano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Uongozi wa KMC unaimani kubwa na Harerimana ambaye awali alikuwa anaifundisha timu ya Lipuli ya Iringa inayoshiriki Ligi Kuu pia.

“Ni kocha ambaye amekidhi vigezo vyote ambavyo tumeweka na uongozi kuamua kuingia naye mkataba. Kupitia yeye, tunaamini timu itafanya vyema na kurejesha ubora wake wa msimu uliopita,” alisema Mwenyekiti wa Bodi ya timu ya KMC, Meya Benjamin Sitta.

Mechi ya kwanza ya Harerimana itakuwa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Uhuru na katika mchezo wa kombe la Azam Sports dhidi ya Pan African ambayo pia itachezwa kwenye uwanja wa Uhuru Januari 24.

Kwa upande wake, Harerimana alisema kuwa amekuja kufanya kazi na kama ilivyo makocha wengi duniani, mafanio ndiyo malengo makuu.

Alisema kuwa anahitaji wachezaji ambao wanajituma na wenye malengo ya kuleta mafanikio kwa timu na vile vile katika kipaji chake.

“Nimekuja kufanya kazi yenye mafanikio, hivyo naomba wachezaji tushirikiane katika kuleta matokeo chanya ya timu na kumaliza ligi katika nafasi nzuri. Nimefurahi kupata uongozi ambao unajali maslahi ya wachezaji na watendaji wa timu,” alisema Harerimana.

Wakati huo huo, Uongozi wa timu ya KMC umefikai makubaliano ya kusitisha mikataba na wachezaji watano kutokana na sababu mbalimbali.

Wachezaji hao ni Aaron Lulambo, George Sangija, Rehani Kibingu, Melly Mongolare na Janvier Besala Bokongu.

Pia mchezaji Vitalis Mayanga ameuzwa kwa timu ya Ndanda FC ya Mtwara.


BENJAMINI SITTA MWENYEKITI WA BODI KMC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...