Na Ripota Wetu, Kimataifa

SERIKALI ya Gambia imemuonya Rais aliyeng'olewa madarakani Yahya Jammeh asijaribu kurejea nyumbani kutoka uhamishoni Equatorial Guinea kwani usalama wake hauna uhakika iwapo atarejea nchini bila ruhusa.

Msemaji wa Serikali ya Gambia ameliambia Shirika la Habari la Uingereza(BBC) leo Januari 13,mwaka 2020 kuwa Msemaji wa chama cha Jammeh alisema anaweza akarejea muda wowote ule.

Nchi jirani za Gambia zilimlazimisha Jammeh kwenda Equatorial Guinea baada ya kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi uliofanyika Disemba mwaka 2016.

Alipoingia madarakani baada ya mapinduzi ya mwaka 1994, aliendeleza mfumo wa uchaguzi wa kawaida lakini baadaye akashutumiwa kwa unyanyasaji wa haki za binadamu ikiwemo mauaji ya kiholela mateso na kukamata watu kiholela.

Mrithi wake Rais Adama Barrow, aliunda tume ya ukweli, maridhiano ya kusikiliza malalamiko ya umma dhidi yake lakini Jammeh amekataa kutoa ushirikiano.

Pamoja na taarifa za Jammeh kuonesha nia ya kurejea nyumbani, imeelezwa mpaka saaa Gambia inachofahamu bado yuko Equatorial Guinea, karibia kilomita 3,000 kutoka nchini Gambia.

Hata hivyo kiongozi wa muda wa chama cha Jammeh, Ousman Rambo Jatta, alikataa kueleza lini hasa kiongozi huyo anatarajiwa kurejea Gambia."Yuko njiani... anaweza kurejea muda wowote tokea sasa," ameambiakipindi cha BBC cha Focus on Africa.

Kwa kukumbusha tu Jammeh alizaliwa Mei mwaka 1965 na aliingia madarakani baada ya mapinduzi mwaka 1994.Mwaka 2013, aliapa kuendelea kusalia madarakani ''miaka bilioni'' iwapo Mungu atampa Umri.

Pia aliagiza hukumu ya kifo dhidi ya wahalifu na wapinzani wake wa kisiasa na mwaka 2007, aliahidi anaweza kutibu Ukimwi na ugumba kwa kutumia dawa za mitishamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...