Na Yassir Simba, Globu ya Jamii

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Luc Eymael amemuonya kwa mara ya mwisho mshambuliaji wa klabu hiyo Bennard Morrison mwenye jezi namba 33 mgongoni kuacha kuuchezea mpira na badala yake ajikite katika kutimiza majukumu yake uwanjani.

Hayo yamesemwa mara baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mpambano wa Azam Sports Federation Cup ( ASFC)  zilizowakutanisha Yanga wananchi dhidi ya maafande wa Jeshi la Magereza Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya

Ambapo iliwachukua Yanga dakika 10 za mchezo katika kipindi cha kwanza kuwagomea maafande wa Tanzania Prisons  kwenda korokoroni mara baada ya beki wa Prisons kuunawa mpira katika kisanduku na hivyo muamuzi wa mchezo huo kuamuru adhabu ya penati ipigwe na mshambuliaji wa Yanga Benard Morisson akaipatia timu yake bao la utangulizi.

Mnamo dakika ya 63 katika kipindi cha pili  mshambuliaji wa Yanga aliyeingia kuchukua nafasi ya David Molinga , Yikpe aliipatia Yanga bao la pili katika mchezo huo akiunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na mfungaji wa bao la kwanza Benard Morrison na kupelekea mchezo huo kumaliza kwa Yanga kuibuka kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Tanzania Prisons

Mara baada ya mchezo huo Yanga imesonga mbele katika hatua inayofuata ya 16 bora ya mashindano hayo na itakutana na timu ya Gwambina kutoka Misungwi mkoani Shinyanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...