Kituo cha Daladala cha Makumbusho jijini Dar cha hitaji matengenezo hivi ndivyo kilivyo.
 Hali ilivyo katika kituo cha Daladala cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa baadhi ya maeneo ya kituo cha Makumusho jijini Dar es Salaam yalivyoharibika.


MADEREVA wa Daladala za kutoka maeneo mbalimbali na kuishia katika kituo cha Makumbusho walalamikia ubovu wa kituo cha daradarahicho jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza na Michuzi Blog moja ya Dereva ambaye hakutaka jina lake litajwe katika mtandao huu, amesema kuwa Mwekezaji na manispaa ya Kinondoni wanamgogoro  na manispaa ndio maana kituo cha daradara cha Makumbusho hakikarabatiwi kwa wakati na kusababisha daradara zinazoingia na kutoka katika kituo hicho kupata wakati Mgumu huku kituo hicho kikiwa na mabonde na mashimo yanayotuamisha maji.

Amesema kuwa mapato kila siku yanakusanywa lakini hawaoni maboresho ya kituo hicho.

" Kila siku na kila daradara inayofika katika kituo hiki lazima tutoe 'buku' Shilingi elfu moja ambapo fedha hizo zinaenda moja kwa moja katika Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni kama hakuna mgogoro kwanini wasikarabati sisi tufanye kazi kwa raha?.

Hata hivyo kituo hicho cha Daladala kinaonekana kuharibika na kutuamisha maji kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha katika kituo hicho.

Mwandishi wa habari hii akapata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa serikali za mitaa za Makumbusho, Felicianus Kamkala, naye alikuwa na haya ya kusema ingawa moja ya majukumu yake ni kisimamia makusanyo na mapato ya eneo la Makumbusho, amesema kuwa yeye kama Mwenyekiti wa eneo hilo anafahamu kuwa mapato ya kituo hicho yanaenda Moja kwa moja katika manispaa ya Kinondoni lakini kuhusu zinatumikaje Meneja wa kituo hicho ndio anajua.

Kwa upande wa Meneja wa kituo cha Daladala cha Makumbusho, Zahoro Hanuna amesema kuwa kituo cha Daradara cha Makumbusho kipo mbioni kujengwa kwani badjeti ya 2020/2021 ndio inayosubiriwa kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho.

Kuhusiana na mgogoro uliopo kati ya mwekezaji na manispaaa amesema mgogoro huo haupo kabisa kati yao, ila kinasubiriwa ni makusanyo yakabilike ndio kituo hicho kifanyewe ukarabati.

Amesema kuwa kituo cha Daladala cha makumbusho kinamiaka sita tuu lakini kimeshaanza kuharibika wako kama manispaa watakiboresha zaidi pale bajeti itakapo toka.

Nilipomuuliza kuhusu bajeti kiasi gani itakarabati kituo hicho. Amesema kuwa kituo hicho kitakarabatiwa kwa bajeti ya shilingi milioni 651.

Kwa siku amesema wanakusanya kuanzia shilingi laki tano hadi laki saba hii ni kwa siku zisizokuwa na hali ya mvua.

Kwa upande wa makusanyo yanakusanywa kwa katika kituo hicho cha Daradara. Amesema kuwa kwa mwenzi wanakusanya kuanzia milioni 17 hadi milioni 20 hii ni kwa kipindi cha miezi isiyokuwa na hali ya hewa ya mvua.

Kwa upande wa miezi ya hali ya hewa ya mvua wanakusanya kuanzia milioni 3 hadi Milioni 4 kwa kuwa Daladala nyingi kipindi cha mvua zinaharibika na hazifiki kituoni na ndicho kipindi ambacho risiti haziuziki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...