Na Karama Kenyunko,Michuzi Globu ya jamii

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi katika kesi hiyo umebakiza maeneo machache kukamilika.

Wakili wa serikali, Easter Martin amedai hayo leo Januari 13, mwaka 2020 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtea

"Mheshimiwa kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa upelelezi bado haujakamilika ila tuko katika hatua za mwisho, bado maeneo machache ili kukamilisha,"amedau.

Hata hivyo hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 27,mwaka 2020 na mshtakiwa Kabendera amerudishwa rumande.

Katika tarehe iliyopita, upande wa mashtaka alieleza Mahakama kuwa, mwenendo wa kesi, upelelezi unaendelea na shauri limefikia hatua nzuri ya maelewano baina ya mshitakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP).

Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173. Inadaiwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Pia inadaiwa katika kipindi hicho, bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh.173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...