Charles James, Michuzi TV
JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limefanikiwa kukamata watu wawili katika kijiji cha Kisima Cha Ndege Wilaya ya Bahi wakiwa na nyara za serikali na kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Watu hao wamekamatwa na pembe moja ya Nyati, ngozi ya mnyamapori aina ya Tandala, silaha aina ya Gobore na gongo la mti linaloandaliwa kuunda silaha aina hiyo ya gobore.
Akizungumza na wandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Giles Muroto amesema pamoja na kukamata nyara hizo za serikali pia wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wa makosa mengine mbalimbali katika msako ambao uliendeshwa na Jeshi hilo.
Kamanda Muroto amesema kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji wamefanikiwa pia kukamata wahamiaji haramu watano na watanzania wawili waliokua wakiwasafirisha kutumia Basi lenye namba za usajili T 963 DWV mali ya Kampuni ya Machimula linalofanya safari zake Arusha na Kondoa.
Msako mwingine uliendeshwa kwa kushirikiana na Barasa la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambapo walifanikiwa kukamata watuhumiwa 25 waliokua wakiuza shehena ya mifuko mbadala iliyo chini ya viwango ipatayo 1550 na vifungashio vya plastiki 599,850 vilivyopigwa marufuku.
" Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma pia tuliendesha msako katika kijiji cha Chenene wilayani Chamwino ambapo tulimkamata Edward Filipo kondakta wa Basi la Kampuni ya Kondoa Line akisafirisha madawa ya Hospitali na vifaa tiba bila kuwa na nyaraka halali.
Pia tunamshikilia Joshua Elisha ambaye ni mlinzi wa Kampuni ya KK akiwa na Compressor ya Friji ambayo aliiba baada ya kuvunja stoo ya lindo analolinda. Tulimkamata akiwa kwenye pikipiki yake kuelekea alipokua akielekea nyumbani, " Amesema SACP Muroto.
Kamanda Muroto ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pale wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu kwenye maeneo yao.
" Niwatake wamiliki wa Kampuni za Ulinzi kuajiri watu ambao ni waadilifu kwani kitendo cha baadhi yao kujihusisha na tabia za wizi kinaleta picha mbaya kwa tasnia ya ulinzi," Amesema Muroto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto akionesha mifuko mbadala iliyokamatwa kwa kushirikiana na NEMC ambayo imetengenezwa chini ya kiwango.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto akizungumza na wandishi wa habari leo ofisini kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto akionesha silaha aina ya Gobore ambalo Jeshi la Polisi limekamata ikimilikiwa kinyume na sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto akionesha compressor ya Friji walioikamata ikidaiwa kuibwa na Mlinzi wa Kampuni ya KK maeneo ya Area D jijini Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto akionesha vifungashio vya plastiki vilivyopigwa marufuku ambavyo wamevikamata.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto akionesha pembe ya nyati ambayo wameikamata.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...