Mwenyeketi wa bodi ya Taasisi CAMFED Jeanne  Ndyetabura (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari, namna taasisi hiyo inavyoshirikiana na serikali katika kuboresha mazingira rafiki kielimu nchini kwa watoto wa kike, hayo yamezungumzwa leo wakati wa mkutano uliofanyika katika makao makuu ya shirika hilo, jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya CAMFED Tanzania, Lydia Wilbard
 Mkurugenzi wa taasisi ya CAMFED Tanzania, Lydia Wilbard (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano uliofanyika leo katika makao makuu ya shirika hilo, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyeketi wa bodi ya Taasisi CAMFED, Jeanne  Ndyetabura.

Mkurugenzi wa Taasisi ya CAMFED TANZANIA, Lydia Wilbard (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanufaika wa Taasisi hio pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo.

Taasisi ya CAMFED inayojishughulisha na uboreshaji wa mazingira sambamba  na kupiga vita unyanyasaji wa watoto wa kike waishio katika mazingira magumu, inatarajia kuwanufaisha wanafunzi wa kike wapatao 9877 kupitia program wezeshi ikiwemo utoaji wa vifaa vya shule kama Sare, madaftari na chakula.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu (27, Januari 2020)  jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa taasisi hiyo Lydia Wilbard amesema kuwa dunia ikiwa imesherehekea siku ya elimu duniani,  tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka 2005 imetoa msaada wa vifaa, semina na chakula kwa wasichana wapatao elfu 50 katika kugharimia ada, pesa ya mitihani na gharama nyinginezo kabla serikali haijapitisha mpango wa Elimu bure nchini.

Amesema kuwa taasisi ya CAMFED inafanya kazi kwa kushirikiana na serikali kupitia wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, TAMISEMI pamoja na Ustawi wa jamii katika kuandaa makongamano na warsha mbalimbali zenye lengo la kuwajengea wasichana uwezo wa kujisimamia na kutambua haki zao.

Akielezea miongoni mwa manufaa waliyoyapata kama taasisi kupitia uwezashaji huo Bi. Lydia Wilbard amesema kuwa miongoni mwa wasomi waliofaidika na CAMFED wamekuwa wakitoa mafunzo ya stadi za maisha katika maeneo mbalimbali nchini, hasa shule walizosomea ili kuwajengea watoto wa kike uwezo wa kupambana na changamoto zinazowakabili sambamba na kuzitafutia ufumbuzi, hali ambayo ina wapa wanafunzi hao nguvu ya kujiamini kwa kujionea mifano halisi hasa ndani ya vijiji vyao kupitia watoa mafunzo hao.

Shule takribani 471 zimenufaika mpaka sasa kupitia taasisi hiyo kutoka mikoa ya Shinyanga, Tabora, Mwanza na Mara

Aidha ameitaka serikali kuweka nguvu zaidi katika kuondoa vikwazo na changamoto mbalimbali kwa mtoto wa kike ili kupunguza utoro, mimba za utotoni na kukatikiza masomo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya CAMFED, Jeanne  Ndyetabura amesema kuwa ndani ya msichana kuna jamii hivyo CAMFED inawasaidia watoto wa kike ili kuijenga jamii bora ya baadae.

Amewataka wazazi na jamii kutolaumu utoro wa watoto wa kike bali ifuatilie sababu za utoro huo ambazo amezitaja kuwa ni pamoja na vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi, ukosefu wa vifaa na unyanyasaji wa kijinsia.

CAMFED kupitia mtandao wake wa (CAMA) ulioanzishwa mwaka 2014 imekuwa ikiwajengea watoto uwezo wa kujiamini kupitia waandaa mafunzo ambao wamezifikia shule zipatazo 471 mpaka sasa.


Pia taasisi hiyo ina mpango wa kukuza wigo mpana wa utoaji huduma na msaada katika maeneo mbalimbali nchini ambayo hayajafikiwa na huduma hizo hasa watoto wa kike.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...