Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii
SHIRIKISHO la Vyama vya Magonjwa yasiyoyakuambukiza(TANCDA) limetoa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari zinazohusu magonjwa hayo ili kuhakikisha jamii ya Watanzania inapata taarifa sahihi.
Akizungumza leo Januari 31 mwaka 2020 wakati wa utolewaji wa mafunzo hayo, Meneja Mradi kutoka Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoyaambukiza Happy Nchimbi amesema kuwa msingi mkbwa wa kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha waandishi wanauelewa wa kutosha kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na visababishi nyake.
Amefafanua shirikisho hilo lenyewe haliwezi kufikisha taarifa hizo kwa wananchi na kwamba bila kutumia waandishi wa habari ambao wana uwezo wa kufikia wanachi wote katika ngazi zote wenye vipato na wasio na vipato, wa mijini na vijijini.
"Dhumuni kubwa ni kuhakikisha taarifa zitawafikia wananchi kuhusu magonjwa yasiombukiza ni sahihi kwa kukutana na wataalamu wa magonjwa haya, pia kuwakikishia waandisshi wa habari kuwa TANCDA tupo na muda wowote wakihitaji uelewa wa au habari kuhusu magonjwa haya tunawakarisha,"amesema.
Ameongeza kuwa matarajio yao baada ya mafunzo hayo waandishi watakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na kwenda kutoa elimu hiyo kwa jami. "Ni matarajio yetu elimu ambayo itatolewa itasaidia wananchi wengi ambao hawana elimu ya kutosha juu ya magonjwa haya kuipata,"amesema.
Amesisitiza kuwa ndani ya nchi magonjwa haya yapo na yanakuwa kwa kasi sana, mwaka 2012 Steps survey ilionesha asilimia 9 ya wananchi wanaishi na ugonjwa wa kisukari na asilimia 26 ina shinikizo la juu la damu, lakini pia viwango vya ufanyaji mazoezi viko chini sana na ulaji wa matunda na mboga za majani ni mdogo sana.
Wakati huo huo Nchimbi amesema magonjwa hayo yapo na yanapoteza maisha ya wananchi wengi,hivyo ameshauri jamii ya Watanzania kujiepusha kwa kuzingatia mlo ulio sahihi ambao una viwango vidogo vya sukari, chumvi na mafuta.
"Tuwe na utaratibu wa kufanya mazoezi nusu saa kila siku, tujiepushe na matumizi ya pombe na sigara. Pia tuna na utaratibu wa kupima afya zetu mara kwa mara, tusipende kujitibia tukiwa majumbani tuende vituo vya afya kwa tiba sahihi,"amesema Nchimbi.

Meneja Mradi kutoka Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoyakuambukiza
Happy Nchimbi akisikiliza kwa makini bada zilizokuwa zinatolewa na watalaam mbalimbali wakati wa mafunzo hayo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa semina ya mafunzo yanayohusu kuandika habari za magonjwa yasiyoyakuambukiza.Mafunzo hayo yamefanyika leo Januari 31 mwaka 2020 jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakiendelea kupata mafunzo wakati wa semina ya mafunzo ya kujengewa uwezo wa kuandika habari zinazohusu magonjwa yasiyokuambukiza.
Mwanzilishi wa Taasisi ya kutoa elimu ya kisukari Lucy Johnbosco akifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo
Mtaalam wa Chakula na Lishe Marry Materu akizungumzia wakati wa mafunzo hayo kuhusu namna bora ya ulaji wa vyakula ili kuepuka magonjwa yasiyoyakuambukiza mwilini.
Mtalaam wa mazoezi Waziri Ndonde akitoa elimu kwa waandishi wa habari wakati wa semina ya mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Jukwaa la kudhibiti matumizi ya tumbaku nchini Lutgard Kagaruki akiwa kwenye semina hiyo kabla ya kuanza kutoa mada kuhusu madhara ya tumbaku wakati wa mafunzo hayo.
:Profesa Endrew Swai akitoa mada wakati wa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kuandika habari zinazohusu magonjwa yasiyoyakuambukiza.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...