
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Nyasa mh. Altho Komba akizungumza katika kikao cha Baraza la
madiwani la Bajeti lililofanyika katika Ukumbi wa Kepten John Komba
Mbamba-bay wilayani hapa,kushoto na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyasa
Bw Bernad Semwaiko
……………………………………………………………………………………….
Baraza la Madiwani la Halmashauri
ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma limepitisha Mpango na Bajeti ya
TSh.bilioni 24.5 kwa ajili kutekeleza shughuli mbalimbali za Halmashauri
zilizopangwa kufanyika kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Mpango huo umewasilishwa na Kaimu
Afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw. Regius Sanane
katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni katika
ukumbi wa Kepten John Komba , Mjini Mbamba-bay Wilayani hapa.
Bw. Sanane alivitaja vyanzo vya
mapato hayo kuwa ni makusanyo ya mapato ya ndani, Matumizi mengineyo,
Mishahara(PE) na Miradi ya Maendeleo.
Aliongeza kuwa , bajeti hii
inalenga ya kujenga msingi imara na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya
viwanda, kuharakisha maendeleo endelevu, kuboresha hali ya maisha na
ustawi wa jamii, na kuharakisha ustawi wa jamii utakaopunguza umaskini
haraka.
Aidha,aliyataja malengo mengine
ni Kuinua ari ya utendaji kazi wenye tija na ufanisi,kuweka na
kuimarisha ushiriki wa wadau wa ndani katika kupanga na kutekeleza
mipango mbalimbali na kutmia uwepo wa mazingira mazuri ya nchi yetu
kuimarisha shughuli za biashara kwa lengo la kuifanya Taifa letu kuwa
Mhimili wa uzalishaji na kitovu cha biashara.
Maeneo mengine ambayo bajeti
imezingatia ni ujenzi wa miundombinu ya Elimu ya Msingi na Sekondari,
kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya, pamoja na kuongeza uzalishaji
mazao ya biashara likiwemo,zao la kahawa,korosho na kokoa.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri
Mh. Altho komba ametoa wito kwa wataalam kuendelea na mchakato wa
kuiwasilisha bajeti hii sehemu zinazohusika kwa kuwa Baraza la madiwani
limeshapitisha ,na Bajeti hii inalenga kutatua Kero za Wananchi wa
Wilaya ya Nyasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...