Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, akimkabidhi kitabu Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB- Ruth Zaipuna wakati wa hafla ya kutambulisha na kutia saini kitabu chake iliyofanyika jijini Mwanza.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB - Ruth Zaipuna akitoa mada kuhusu ubinafsishaji wa benki hiyo wakati wakati wa hafla ya utambulisho wa kitabu cha "My Life, My Purpose" kilichoandikwa na Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa katika picha ya pamoja na uongozi wa Benki ya NMB.
Mkapa afurahia uamuzi kuibinafsisha Benki ya NMB
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa amesifu uamuzi wa Serikali yake
kwa kuamua kuibinafsisha Benki ya NMB.
Akizungumza jijini Mwanza juzi
wakati wa hafla ya kutambulisha kitabu chake cha: My Life, My Purpose – (Maisha
Yangu, Dhamira Yangu), Rais huyo Mstaafu alisema suala la ubinafsishaji taasisi
hiyo ulitokana na uamuzi wa mwanzoni mwa utawala wake mara baada ya kuingia
madarakani mwaka 1995.
Ilipofika mwaka 1997, Serikali
ya Rais Mkapa iliamua kuundwa kwa Benki ya NMB baada ya kugawanywa kwa
iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
Baada ya kuundwa kwa NMB mwaka
1997, mwaka 2005 serikali ya Rais Mkapa iliuza asilimia 49 ya hisa za NMB kwa
wawekezaji wa Rabobank ya Uholanzi.
“Nafarijika kuona NMB ni
miongoni mwa mabenki makubwa yenye mtandao mkubwa nchini ikihudumia wananchi wa
kawaida hadi vijijini,” alisema Mkapa
Akionyesha
kuchukizwa na wanaokosoa uamuzi wa ubinafsishaji uliochukuliwa na serikali
yake, Rais Mkapa alisema watu wanatakiwa kuelewa kuwa wakati huo ilikuwa ni
lazima kufanya uamuzi ili kuokoa pesa za walipakodi zilizokuwa zikipotea kwa
kutolewa kama ruzuku ya kuendeshea mashirika ya umma.
Ndani
ya kitabu chake, kuna aya inayosema wanaokosoa uamuzi wa ubinafsishaji
wanapaswa kuelewa kuwa wakati huo, mashirika ya umma yalikuwa na hali mbaya
kifedha kiasi kwamba serikali ililazimika kutumia kiasi kikubwa cha pesa za
walipakodi kugharamia uendeshaji wa mashirika hayo. “…hiyo siyo kazi moja wapo
ya pesa za serikali,” anaandika Mkapa.
Akizungumzia mafanikio ya benki
hiyo, Kaimu Mkurgenzi Mtendaji wa NMB, Ruth Zaipuna alisema kwa kipindi cha
miaka 22 iliyopita, benki hiyo imejipambanua kuwa mfano bora wa uamuzi wa
ubinafsishaji baada ya kufikia kuwa kimbilio la wafanyabiashara wadogo, kati na
wakubwa kwa mitaji na ushauri wa kitaalam.
Kwa
miaka 22 ya uwepo wake, Benki ya NMB imetoa jumla ya Shilingi trillioni 1.2
kusaidia biashara ndogo na za kati na mikopo mingine Shilingi trilioni 2.2
kusaidia wateja binafsi.
Katika
kusaidia wakulima, Bi. Zaipuna alisema mwaka huu wa 2020, Benki imepanga
kufungua akaunti zaidi ya 300,000 za wakulima ili kuhakikisha kuwa wakulima
wanapata malipo yao kupitia mfumo rasmi wa fedha na hivyo kuchangia katika
kukuza huduma jumuishi za fedha (financial inclusion) hapa nchini.
Bi.
Zaipuna alisema Benki ya NMB imeendeleza ushirikiano wake na Mfumo wa Kielektroniki wa
Malipo ya Serikali (Government's electronic payment system – GePG),
ambapo mpaka hivi sasa taasisi 590 za serikali zimeunganishwa katika mfumo huo.
Kupitia mfumo wa GePG, Benki ya NMB huwezesha kukusanya kwa jumla ya mapato ya
serikali yapatayo Shilingi trilioni 2.1.
“Tunafanya
hivyo kwa kutambua kuwa ni wajibu wetu kuunga mkono miradi ya kimkakati ya
serikali. NMB ndiyo iliyokuwa benki ya kwanza kuunganishwa na mfumo wa GePG,”
alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...