Mkuu wa Chuo cha Kamandanti Brigedia Jenerali Venanti Rutashobya akikata mfuko uliowekewa mche wa mti kabla ya kuupanda katika eneo la chuo hicho kilichoko Kikosi cha 671 Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Kamandanti Brigedia Jenerali Venanti Rutashobya akipanda mti kwenye eneo la chuo hicho.
Mmoja wa maofisa wa Chuo cha Kamandanti kilichopo kikosi cha 671 akipanda mti.
Ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Chuo cha Kamandanti akipanda mti katika eneo hilo la chuo.
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Francis Kiondo akipanda mti katika eneo la Chuo cha Kamandanti.
Mmoja wa watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Wilaya ya Temeke akipanda mti huku akisaidiwa na moja ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)
Mmoja wa maofisa wa JWTZ katika Chuo cha Kamandanti akishiriki kupanda mti.
Mtumishi wa TFS Wilaya ya Temeke akipanda mti katika eneo la Chuo cha Kamandanti kilichopo kikosi cha 671 Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa askari wa JWTZ katika Chuo cha Kamandanti akipanda mti chuoni hapo.
Ofisa wa JWTZ akiendelea kupanda mti katika chuo hicho.(PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE).

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii



MKUU wa Chuo cha Kamandanti katika Kikosi cha 671 Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam Brigedia Jenerali Venanti Rutashobya amewaongoza maofisa na askari wengine wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kupanda miti chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya kutunza na kuboresha mazingira.



Ametumia nafasi hiyo kusisitiza wataendelea kupanda miti ili kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri na hewa safi huku akitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti na kutunza mazingira.



Akizungumza wakati wa upandaji miti katika  chuo hicho, Brigedia Jenerali Rutashobya kwanza amewapongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilaya ya Temeke kwa kupeleka miche ya miti chuoni hapo na kushiriki kikamilifu kuipanda.



"Kipekee nawapongeza TFS Wilaya ya Temeke kwa kutupatia miche hii ya miti ambayo leo tumeipanda hapa chuoni kwetu, tutahakikisha tunaitunza ili ikue na kuleta mandhari nzuri ya hapa chuoni kwetu.Tumeamua kupanda miti hii kwa kutambua huu ndio wakati wake na tutaendelea kupanda kadri tutakavyoweza,"amesema.



Kwa upande wake Meneja wa TFS Wilaya ya Temeke Dar es Salaam Francis  Kiondo amesema miti ambayo imepandwa chuoni hapo ni sehemu ya miche 500,000 iliyotengwa kwa ajili ya kupandwa katika katika wilaya zote za Jiji hilo.



"TFS Wilaya ya Temeke tumepewa dhamana ya kuotesha miche ya miti 500,000 itakayopandwa jijini Dar es Salaam, kila Wilaya tunatarajia itachukua miti 100,000. Leo tuko katika chuo hiki cha jeshi ili kupanda miti, ndugu zetu kwa kutambua umuhimu wa miti walikuja kwetu na kutueleza kuwa wanaomba miti ili kupanda katika chuo chao, nasi tumefanya hivyo,"amesema.



Pia amesema uboreshaji wa mazingira ni kwa maeneo yote yakiwemo yanayohusu vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama huku akifafanua kuna faida nyingi ya kupanda miti ikiwemo ya kusaidia kuondoa hewa ukaa.



Kuhusu wananchi wanaohitaji kupanda miti katika maeneo yao wanachotakiwa ni kufika ofisi za TFS katika wilaya husika na kisha wataonana na mameneja ili wapatiwe miti.Amesema kuna aina nyingi za miche ya miti ambayo wanayo ikiwemo ya kivuli ,mbao, maua na matunda na kueleza bustani yao ya miche ya miti iko Vikindu jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...