Maofisa Waandikishaji  wa mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (ICHF)  Wilaya ya Tandahimba  wamepewa mafunzo ya  ukusanyaji  wa fedha kwa njia ya kielektroniki

Akizungumza  kwenye ukumbi wa Halmashauri Mratibu wa ICHF Violeth Mahembe  alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kutokuwepo ucheleweshaji Kama ilivyo awali

Alisema awali Waandikishaji walikuwa wanapeleka   kuweka fedha kwenye akaunti  hivyo kusababisha ucheleweshaji lakini sass   itawarahisishia na  fedha inayopatikana kwenda sambamba na kaya alizosajili

"Sasa hivi Ofisa Mwandikishaji wa ICHF hatakwenda kuweka fedha benki Bali fedha zote zitaingizwa kwenye mfumo wa serikali kwa njia ya kielectronik," alisema Mahembe

aidha alisema kuwa  mafunzo hayo pia yanawahimiza Waandikishaji kuweza kuhamasisha wananchi kujiunga na ICHF iliyoboreshwa ili kuweza kupata  huduma za kiafya kwa unafuu kwa kuwasajili kwa njia ya mtandao ( IMS)

Naye Ofisa Mwandikishaji wa Kijiji Cha Mchangani Kata ya Mkoreha Zainabu Linyono alieleza kuwa mafunzo hayo yamewasaidia na watakwenda  kufanya kazi kwa ufanisi zaidi

"Kwakweli njia hii itapunguza ucheleweshaji wa kuweka fedha kwakuwa wengine tunakaa vijijini moja ya sababu zilikuwa zinatufanya kutoingiza kwa wakati ," alisema Linyono.

 Mratibu wa ICHF Wilaya ya Tandahimba Violeth Mahembe
 Maofisa Waandikishaji wa mfuko wa afya ICHF wakisikiliza mafunzo
 Washiriki wakisiliza kwa makini
 Mwezeshaji Cleophace Maulambo akifafanua Jambo kwa washiriki wa mafunzo ya ICHF

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...