Shughuli zinazofanywa na binadamu ndani ya Mito zimetajwa kuwa changamoto kubwa katika Mito wilayani Kinondoni kutokana na kuzungukwa na makazi ya watu pamoja na mito hiyo kupita kando kando ya makazi hayo.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Daniel Chongolo alipotembelea Mto Tegeta uliopo jiji la Dar es Salaam, Chongolo amesema Wilaya ya Kinondoni ina dhamana yakulinda haki za Wananchi wote wanaoishi kando kando ya Mito hiyo kwa kufuata Sheria ya Mita 60  pamoja na wale wanaochota Mchanga ndani ya Mito hiyo kuhakikisha wanachukua tahadhari kuzuia kuondoka wa udongo na athari za Mto husika.

"Kama atatokea mtu anachimba mchanga katika eneo hili kwa lengo lakutafuta Pesa basi na sisi kama Mamlaka husika tutamlinda yule anayeishi kando kando ya Mto, sisi tunatengeza haki na wajibu", amesema Chongolo.

Afisa Maji, Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, Simon Ngonyani amesema nia ya Bonde hilo na Mkuu wa Wilaya kufika katika eneo hilo la Mto Tegeta ni kuratibu zoezi  la uchotwaji wa Mchanga kwa utaratibu Mzuri ili kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake na kulinda Mto.

Ngonyani ametoa wito kwa Wananchi kuepuka kujenga Nyumba zao kando kando ya Mabonde ili kunusuru nyumba hizo kusombwa na Maji vipindi ambavyo mto unajaa zaidi.

"Nia yetu kuja hapa Mto Tegeta, sio mbaya tumekuja kuwekana sawa tu kuhusu uchimbaji mchanga katika eneo hili, tukifanya vibaya nyumba zote katika eneo hili zitasombwa na maji ya mto", amesema Ngonyani.

Kwa Upande wao Wananchi wanaosomba mchanga katika eneo hilo wametoa malalamiko yao kwa Mkuu wa Wilaya huyo kuhusu mgogoro uliopo kati yao na Kandarasi zinazochota Mchanga katika Mto Tegeta.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza na Dereva wa Gari la kuchimba mchanga maarufu kama Caterpillar linalosomba mchanga katika eneo hilo kwa utaratibu wakuondoa mchanga huo ili kuzuia athari katika Mto Tegeta (Salasala) jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Mto Tegeta (Salasala) iliyopandwa Mimea aina ya Mianzi ili kuzuia mmomonyoko wa udongo katika eneo hilo la Mto.


Athari ya mmomonyoko wa udongo katika moja ya Nyumba iliyopo eneo la Mto Tegeta (Salasala) jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...