Na Amiri kilagalila-Njombe

Mamia ya wananchi wamejitokeza hii leo katika viwanja vya jeshi la polisi mkoani Njombe kuaga miili ya askari watatu waliofariki katika ajali mapema alfajiri ya tarehe tatu ambapo ajali hiyo imehusisha basi la abiria kampuni ya sharon lenye namba za usajiri T349 CXD na gari la polisi lenye namba za usajili pt 3734.

Askari waliofariki katika ajali hiyo ni namba H 4401 Marianus Said Hamissi,namba H6802 pc Michael Mwandu na askari namba H 7486 pc Hery Athmani ambapo wote wamesafirishwa kuelekea makwao kwaajili ya mazishi

Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari hao mkuu wa mkoa wa Njombe Cristopher Ole Sendeka amesema, serikali imepoteza vijana mhimu ambao wamefariki wakati wakienda kulitumikia taifa na kuwataka askari wengi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

“Ajali hii imeondo vijana wetu watatu,wawili wapo Moi tumewakimbiza jana kwa ndege na wengine wapo kwenye hospitali yetu ya kibena na hakika vyombo vyote vitasimamia kujua ukweli wa tukio hili na aliyefanya dhambi hii kwa uzembe atachukuliwa hatua za kisheria”alisema Ole Sendeka

Hamis Issa ni kamanda wa polisi mkoa wa Njombe amewashukuru wakazi wa mkoa wa Njombe kwa kujitokeza kwa wingi pamoja na kujitolea michango yao kuhakikisha askari wote waliofariki wanasafirishwa kuelekea kwao kwaajiri ya mazishi.

“Wananchi mmeonyesha ni jinsi gani mna upendo na vijana wenu,na hawa waliofariki kwa kweli wamefariki wakiwa wanaenda kutimiza jukumu la kisheria,tunawashukuru sana”alisema Hamis Issa

Solanus Mhagama ni mmoja wa wakazi mkoani hapa ameonyesha kusikitishwa na kifo cha askari hao ambao walikuwa bado vijana wadogo na hivyo kuiomba serikali kuweka matuta pamoja na kutanua barabara hiyo ili kuepusha ajali katika eneo hilo ambalo lina mlima mkali.

Ajali hiyo iliyosababaishwa na mwendokasi wa gari ya abiria ilipelekea vifo vitatu vya askari wa polisi kikosi cha kutuliza gasia mkoani Njombe huku wengine tisa wakiendelea na matibabu katika hospitali ya mji Njombe Kibena na hospitali ya taifa Mhimbili.

Ibada ya kuagwa miili hiyo imehudhuliwa na viongozi wa dini mbalimbali ambapo wametumia fulsa hiyo kuwa taka wananchi kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazosababishwa na uzembe.
 Miili ya akari watatu wa jeshi la polisi mkoani Njombe ikiwa mbele ya mamia ya wananchi kwa ajili ya kuagwa mapema siku ya leo kupelekwa makwao kwa mazishi
 Baadhi ya askari wa polisi kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wamebeba moja ya miili na kupeleka kwenye usafiri kwa ajili ya kusafirishwa.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka wakati akipita mbele na kuaga miili ya askari.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kuaga miili ya askari watatu waliofariki kwa ajali.
  Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akishindwa kuzuia hisia zake wakati alipotaka kuzungumza jambo na kuwashukuru wananchi wa Njombe kwa kujitokeza katika kuaga miili ya askari watatu waliofariki kwa ajali
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuaga miili ya askari wa jeshi la polisi mkoani Njombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...