Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa
Njombe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri (kushoto)
akisalimiana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii
Imelda Kamugisha(kulia)alipokuwa akipokea msafara wa kijinsia wa
kutokomeza ukatili.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii Imelda Kamugisha akielezea lengo la msafara wa
kijinsia wa kutokomeza ukatili wakati msafar huo ulipowasili mkoani
Njombe.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa
Njombe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri akizungumza
na wananchi wa Makambako alipokuwa akiupokea msafara wa kijinsia wa
kutokomeza ukatili.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa
Njombe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri akiangalia
bidhaa za wanawake wajasiriamali alipokuwa akipokea msafara wa kijinsia
wa kutokomeza ukatili.

MsaniiNurdin Bilal ‘Sheta’
akitumbuiza katika mji wa Makambako wakati Msafara wa kijinsia
uliposimama mkoani Njombe katika kutoa elimu juu ya mapmbano ya vitendo
vya ukatili wa kijinsia.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia msafara wa ukatili wa kijinsia katika mji wa Makambako mkoani Njombe.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu Makambako
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth
Msafiri ameagiza kukamatwa kwa walimu mkoani Njombe watakaobainika
kuwafanyia vitendo vya kikatiki wanafunzi ili kukomesha vitendo hivyo
vinavyoendelea kutoka nchini.
Hayo yamebainika leo Makambako
mkoani Njombe wakati msafara wa kijinsia kutokomeza ukatili ulipofika
mkoani humo kwa ajili ya kutoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya
wanawake na watoto.
Mhe. Ruth amesema kuwa Serikali
haipingi adhabu ya viboko ila sio kutoa adhabu ya viboko vya kupitiliza
na kusababisha vilema na maumivu kwa wanafunzi.
Ameongeza kuwa suala la ukatili ni
mapambano makubwa nchini hivyo jitihada zinahitajika kwa wananchi wadau
na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha wanaunganisha nguvu
pamoja kuondokana na vitendo vya ukatili.
Mhe. Ruth amevitaka vyombo vya
usalama kuacha kufanya ukatili kwa kuchelewesha kesi za vitendo vya
ukatili wa kijinsia na kusababisha ukatili wa kihisia kwa wahanga wa
vitendo hivyo.
“Vyombo vya usalama mnachelewesha
kesi mnaomba rushwa nawaomba vyombo vys usalama msiwe kikwazo cha
kutopatikana kwa haki ya wahanga wa vitendo vya ukatili” alisema.
Akizungumza kuhusu msaada wa
kisheria unaotolewa na Shirika la Legal Serivces Facility Joseph Magazi
amesema kuwa wameweka nguvu katika kuisidia jamii katika matatizo ya
kisheria kwa kuwawezesha wasaidizi wa kisheria katika mikoa na wilaya
kutoa elimu husika.
“Tumejipanga kushirikiana na
Serikali katika kuhakikisha tunaifikia jamii katika kutoa elimu
itakayowezesha wenye matatizo mbalimbali ya kisheria kupata msaada na
kuyatatua matatizo yao” alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...