KATIBU MKUU Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi za Wakurugenzi za OSHA na VIPIMO (Weights & Measures), Dkt. Adelhelm Meru (Kushoto), akipokea kitabu cha "MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY" kutoka kwa mwandishi wa Kitabu hicho, Ndg. Derek Murusuri, jijini Dar es Salaam leo (13Feb., 2020). Kitabu hicho cha kwanza kuihakikishia Afrika, pasina shaka kuwa inaweza kuongoza uchumi wa dunia, kilizinduliwa mwezi uliopita (January, 2020) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda.

Dk. Meru ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, na Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, amempongeza Murusuri na kumtaka akisambaze kitabu hicho katika mataifa mbalimbali ya Afrika ili kuleta hamasa na ari mya kwa waafrika waweze kuongeza juhudi na ubunifu katika kazi ili kufikia uchumi shindani duniani. Amesema kitabu hiki kimekuja wakati mwafaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...