KAMPUNI ya matangazo ya kidigitali barani Afrika "Startimes" wameendelea kutoa maudhui mbalimbali kupitia tamthiliya mbalimbali na leo Februari 13 wamezindua tamthiliya mpya inayokwenda kwa jina la "Razia Sultan" na hiyo ni mara kabla ya kumalizika kwa tamthiliya ya "Waaris" ambayo ipo ukingoni na wateja wengi wamekuwa wakifuatilia tamthiliya hiyo iliyobeba maudhui ya kuelimisha na kuburudisha.

Akizungumza katika ufunguzi huo Meneja masoko wa Startimes David Malisa amesema kuwa wamekuwa wakijaribu kuleta vitu vya tofauti ili kuweza kukidhi mahitaji ya wananchi;
" Tumezingatia soko la ushindani, kwenda na wakati na tunaendelea kuongeza maudhui mbalimbali yatakayokidhi mahitaji ya wateja" ameeleza Malisa.

Aidha amesema kuwa tamthiliya hiyo ya Razia Sultan imebeba burudani na mafunzo ambayo kwa namna moja au nyingine wateja na watazamaji watapata mafunzo mbalimbali kupitia binti Razia ambaye amepitia shida mbalimbali katika kupambania maisha yake.

Amesema kuwa Startimes itaendelea kutoa maudhui kwa watu wa rika zote wakiwemo watoto na hiyo ni pamoja na kupunguza bei za dikoda zao ili kutoa nafua kwa wateja wao.
Meneja masoko wa Startimes David Malisa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa wamezindua tamthiliya mpya inayokwenda kwa jina la "Razia Sultan" na hiyo ni mara kabla ya kumalizika kwa tamthiliya ya "Waaris"  uliofanyika katika ukumbi wa Sinema uliopo Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa tamthilia hapa nchini wakimsikiliza Meneja masoko wa Startimes David Malisa alipokuwa anazungumza na waandishi was habari wakati wa wamezindua tamthiliya mpya inayokwenda kwa jina la "Razia Sultan" na hiyo ni mara kabla ya kumalizika kwa tamthiliya ya "Waaris"
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...