Katika kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally amekabidhi  mashine ya photokopi yenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kwa mzee Shabani Kanijo (73) ambaye ni mstaafu katika kitengo cha Tehama CCM makao Makuu.

Mzee huyo alikuwa ni mtumishi wa CCM tangu mwaka 1965 na alistaafu mwaka 2004, ambapo baadae alianza kusumbuliwa na maradhi na shughuli zake nyingi za kujipatia kipato zikasismama kwa muda mrefu.

Mapema mwaka huu Mzee Kanijo alifika Ofisi ya Katibu  Mkuu kuomba msaada hasa unaohusiana na taaluma yake ili aweze kujimudu na kujiendesha baada ya afya yake kuanza kuimarika, ambapo ombi lake kubwa lilikuwa ni kupata mashine ya kuchapa (Photocopy) kwa ajili ya kufufua steshenari yake iliyokuwa imesimama kwa kipindi chote cha ugonjwa.

Kama ilivyo utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi kuwa karibu na makundi mbalimbali ya watu wenye uhitaji hasa wazee, leo tarehe 05 Februari, 2020 Makao Makuu ya CCM,  Dkt. Bashiru amemkabidhi vifaa vyote vya steshenari  ambapo mzee huyo ameishukuru CCM na kueleza kuwa,

“ninaishukuru sana CCM kwa kuendelea kuwa karibu na sisi wazee, lakini zaidi naipongeza kwa kufanya mambo ambayo wakati wote yalikuwa yakipigiwa kelele na wananchi, sasa hata wapinzania hawana ajenda  tena.”

Ameongeza  kwa kuuliza kuwa,’’ Hao wapinzania wanataka nini tena? Kama hata wao mambo waliokuwa wanayataka CCM chini ya Rais Magufuli  imeyafanya yote.”

Aidha Katibu Mkuu amesisitiza kuwa, ni vema vifaa hivyo ama msaada wowote unaotolewa na Chama utumike kwa malengo yaliotarajiwa na sio vinginevyo ili msaada huo uwe na tija na Chama kiendelee kusaidia wengine zaidi kwa kadri ya uwezo na mahitaji ya wenye uhitaji.

Ikumbukwe kuwa, leo ni siku ya kuzaliwa kwa CCM ambapo Chama hiko kinatimiza miaka 43 tangu kuundwa kwake kutoka vyama vya ukombozi vya TANU na ASP terehe 05 Februari, 1977.
  Katibu MKuu wa CCM (hayupo pichani) Dkt Bashiru Ally akizungumza jambo na Mzee Shabani Kanijo (73) ambaye ni mstaafu katika kitengo cha Tehama CCM

 Mzee Shabani Kanijo (73) ambaye ni mstaafu katika kitengo cha Tehama CCM makao Makuu akieleza jambo kwa Katibu MKuu wa CCM (hayupo pichani) Dkt Bashiru Ally alipokuwa akizungumza nae.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...