Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Ruth Massam (kushoto) akiwakabidhi vitu mbalimbali  wauguzi wa  Taasisi ya Mifupa (MOI), iliyopo kwenye  Hospitali ya Taifa Muhimbili   wanaohudumia  watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa ambao wanapata matibabu  hospitalini hapo.
Afisa Ustawi wa Jamii  Mwandamizi kutoka  katika taasisi hiyo, Bw. Frank Matua akitoa taarifa fupi kuhusu watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Mhe. Martha Mpaze akishusha vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo  kwa ajili ya kusaidia watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa wakiwemo mama zao ambao wanapata matibabu katika  Taasisi ya Mifupa (MOI), iliyopo kwenye  Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Ikiwa ni moja ya huduma waliyoifanya katika kuadhimisha Wiki ya Sheria ya mwaka huu.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Ruth Massam (kushoto) akitoa elimu ya sheria kwa  wakina mama ambao wenye watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa ambao wanapata matibabu   katika Taasisi ya Mifupa (MOI), iliyopo kwenye  Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...