*Ina Madaktari bingwa wa Wabobezi 16 madaktari bingwa 162.
*Yaanzisha Huduma ya Kutibu Kifafa na Degedege.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii,Mwanza

Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando ya Jijini Mwanza  imeijimarisha katika utoaji huduma za afya kwa kipindi cha Miaka minne kutokana na uwekezaji wa Serikali katika huduma hizo .

Hospitali hiyo katika kipindi cha Miaka minne ya serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt.John Magufuli  imekuwa na madaktari bingwa wabobezi 16 pamoja na madaktari bingwa 162.

Akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo  Dkt.Bahati Wajanga amesema kuwa katika kipindi cha Miaka minne wameanzisha huduma za matibabu kwa Magonjwa mbalimbali ikiwemo  Kifafa ,Degedege, Magonjwa ya mfumo wa Chakula na Kifua ,Usafishaji Damu ,Kansa ,Huduma za macho pamoja huduma za Meno.

Dkt.Wajanga amesema katika miaka hivi karibuni walikuwa hawana baadhi ya huduma hizo lakini sasa wanatoa hali ambayo wagonjwa wengi walikuwa wanapata Rufaa kwenda katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Amesema Huduma ambazo wameanzisha katika hospitali hiyo ni kutokana na kuwa idadi kubwa ya wagonjwa lakini kwa sasa wametatua tatizo hilo.
Magonjwa ambayo yalikuwa changamoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Ziwa Bugando ni  Macho,Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Kifua,Magonjwa Kinywa cha Meno pamoja na Kifaa na Degedege.

Amesema Serikali inatarajia kuweka mtambo wa MRI ambapo Jengo lake  limeshakamilika  kwa ajili ya kufunga kwa hivi karibuni.

Dkt.Wajanga amesema kwa mafanikio walioyapata bado kama Hospitali inaebdelea kuwekeza huduma mbalimbali za katika hospitali hiyo  katika kuokoa maisha ya Wananchi kwa utoaji wa matibabu bora ya kuokoa vifo.

"Tumejipanga kutoa huduma bora za Afya katika Hospitali yetu ya Bugando kutokana na serikali kuwekeza sekta ya Afya hivyo kazi yetu ni kutibu kuokoa maisha ya wananchi wetu"amesema Dkt. Wajanga.

Hata hivyo amesema kuwa katika miaka minne wazalisha Maji aina 16 ikiwemo na Maji tiba kwa ajili ya wagonjwa wanaotakiwa kuongezewa maji.
 Daktari Bingwa wa Meno na upasuaji wa Shingo Emmanuel Motega nakueleza namna ya wanavyotibu Meno katika hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando.
 Daktari Bingwa Mbobezi  wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Nini wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando David Maginge akizungumza na waandishi habari namna wanavyoweza kutibu Magonjwa moja kwa moja katika mwili wa binadamu.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Afya,Meandeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Gelard Chami akionesha kuunga Kampeni ya Kifafa katika Kanda ya Ziwa Wakati ziara ya kuangalia mafanikio ya uwekezaji wa Sekta ya afya katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando kwa miaka minne ya Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
 Daktari wa Bingwa wa Macho James Shimba akipima uoni wa Macho Mmoja ya waandishi wakati wa ziara katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando Dkt.Bahati Wajanga akizungumza na waandishi habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto wakati ziara ya kuangalia mafanikio ya uwekezaji wa sekta ya Afya ya Kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya.
 Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando Lucy Mogele akitoa maelezo wakati wa kukaribisha waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto  walipofika kuangalia mafanikio ya uwekezaji wa Serikali  wa sekta ya afya katika  hospitali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...