Mkurugenzi Idara
ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
akisisitiza umuhimu wa Tathmini ya Uharibifu na Mahitaji Baada ya Maafa
kutokea, Jijini Tanga, wakati alipofungua mafunzo ya kuwajengea uwezo
wataalam wanaohusika na Tathmini ambayo huainisha madhara, hasara za
kiuchumi, na gharama za mahitaji ya kurejesha hali baada ya maafa
kutokea..Kulia ni Katibu Tawala wa mkoa huo Noel Kazimoto

Baadhi ya
wataalamu wa menejimenti ya maafa wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea
uwezo wa Tathmini ya Uharibifu na Mahitaji Baada ya Maafa kutokea,
kabla ya kufanya tathmini hiyo katika Halmashauri za mkoa wa Tanga.
Tathmini huainisha madhara, hasara za kiuchumi, na gharama za mahitaji
ya kurejesha hali baada ya maafa kutokea.
Mratibu kutoka
Benki ya Dunia, Nyambiri Kimacha akisisitiza umuhimu wa Tathmini ya
Uharibifu na Mahitaji Baada ya Maafa kutokea, Jijini Tanga, wakati wa
mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wanaohusika na Tathmini kabla ya
kufanya tathmini hiyo ambayo huainisha madhara, hasara za kiuchumi, na
gharama za mahitaji ya kurejesha hali baada ya maafa kutokea.
Baadhi ya
wataalamu wa menejimenti ya maafa wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea
uwezo wa Tathmini ya Uharibifu na Mahitaji Baada ya Maafa kutokea,
kabla ya kufanya tathmini hiyo katika Halmashauri za mkoa wa Tanga.
Tathmini huainisha madhara, hasara za kiuchumi, na gharama za mahitaji
ya kurejesha hali baada ya maafa kutokea
Baadhi ya
wataalamu wa menejimenti ya maafa wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea
uwezo wa Tathmini ya Uharibifu na Mahitaji Baada ya Maafa kutokea,
kabla ya kufanya tathmini hiyo katika Halmashauri za mkoa wa Tanga.
Tathmini huainisha madhara, hasara za kiuchumi, na gharama za mahitaji
ya kurejesha hali baada ya maafa kutokea
Mtaalamu Mshauri
kutoka nchi Ghana, Seth Vordzorgbe, akisisitiza umuhimu wa Tathmini ya
Uharibifu na Mahitaji Baada ya Maafa kutokea, Jijini Tanga, wakati wa
mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wanaohusika na Tathmini kabla ya
kufanya tathmini hiyo ambayo huainisha madhara, hasara za kiuchumi, na
gharama za mahitaji ya kurejesha hali baada ya maafa kutokea.

Wataalam wa
menejimenti ya maafa kutoka ngazi ya Wizara, mkoa, wilaya, na mashirika
yasyokuwa ya kiserikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
mafunzo ya kuwajengea uwezo wa Tathmini ya Uharibifu na Mahitaji Baada
ya Maafa kutokea, kabla ya kufanya tathmini hiyo katika Halmashauri za
mkoa wa Tanga. Tathmini huainisha madhara, hasara za kiuchumi, na
gharama za mahitaji ya kurejesha hali baada ya maafa kutokea.
*******************************
Tathmini ya
Uharibifu na Mahitaji Baada ya Maafa, ni mfumo wa kimataifa uliokubaliwa
kuainisha madhara, hasara za kiuchumi, na gharama za mahitaji ya
kurejesha hali baada ya maafa kutokea. Mfumo huo hutumiwa na mataifa
mengi duniani katika kuainisha athari hizo kwa kuzingatia aina ya
maafa wanayoyapata, ambapo serikali hutambua ni kwa kiwango gani maafa
yamekuwa yakiathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja na pato la
taifa na hivyo kuweka mikakati thabiti ya kuzuia na kupunguza madhara.
Ofisi ya Waziri
Mkuu, Idara ya menejimenti ya maafa imeratibu zoezi la kufanya tathmini
kwa kutumia mfumo huo kwa mara ya kwanza hapa nchini mkoani Tanga kwa
kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa iliyopata maafa ya mafuriko na
kupata madhara makubwa katika sekta za Kilimo, Afya, Elimu, Mazingira na
Miundombinu kufuatia athari ya mvua za vuli za mwezi Oktoba hadi
Desemba, mwaka jana (2019).
Akiongea wakati
wa kufuatilia uratibu wa tathmini hiyo jijini Tanga, Mkurugenzi Idara ya
Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe,
amefafanua kuwa Serikali kwa kushirkiana na benki ya dunia mwaka jana
walitoa mafunzo kwa watalaam wa sekta mbalimbali kwa ajili ya kuwajengea
uwezo wa kitaalamu wa kufanya tathmini hiyo na kwa sasa wanafanya
tathmini kwa vitendo mkoami humo, lengo ni kuwa na wataalamu wenye
uwezo huo kuanzia ngazi za msingi za menejimenti ya maafa.
“Mfumo huu
utatusaidia kupata taarifa ya kina ya madhara, matokeo na rasilimali
zinazohitajika katika kurejesha hali kwa kila sekta iliyoathiriwa, pia
taarifa zake zinasaidia kuandaa mkakati wa kitaifa na wa kimkoa wa
kurejesha hali na hatimaye Kuweka mfumo wa Kitaifa na kimkoa wa
kurejesha hali kwa kipindi cha sasa na baadaye.”Amesisitiza Kanali,
Matamwe.
Kanali Matamwe,
amefafanua kuwa Tathmini hiyo ni shirikikshi kwa maana ya sekta ya umma
na sekta binafsi ambapo wadau wa masuala ya maafa hushirikishwa yakiwemo
mashirika ya umoja wa mataifa, Benki ya dunia na Mashirika yasiyo ya
kiserikali. Aidha, ameeleza kuwa zoezi hilo linalenga kujenga uwezo kwa
vitendo kwa wataalamu kutoka katika ngazi ya wizara, mkoa na wilaya
katika kufanya tathmini ya uharibifu na mahitaji kutokana na maafa kwa
kila sekta.
Naye mwenyekiti
wa Kamati ya Usimamizi wa Maafa, kwa mujibu wa sheria ya Maafa Na.7 ya
mwaka 2015, ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa, akiwakilishwa na Kaimu
Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, Noel Kazimoto amefafanua kuwa mkoa huo
mvua za msimu uliopita wa vuli wa mwaka jana, mkoa huo ulipata athari
zinazojumuisha vifo, uharibifu wa miundombinu ya barabara, maji, na
miundombinu ya kutolea huduma za elimu na afya, pia kubomoka kwa makazi
na kuharibika kwa mfumo wa maisha ya kijamii ya kila siku.
Aidha, ameongeza
kuwa, Tathmini hiyo itaujengea uwezo mkoa huo kuandaa mipango na
mikakti ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu katika kurejesha hali
katika ubora zaidi, kwa kuwa imejikita katika kuangalia madhara
yaliyojitokeza katika sekta ya elimu, afya, kilimo, makazi, miundombinu
pamoja na huduma za maji na usafi. Vilevile tathmini hiyo imeangalia
masuala mtambuka, kama vile mazingira, masuala ya upunguzaji wa athari
za maafa na usawa wa kijinsia.
Tathmini hiyo
iliyofadhiliwa na Benki ya Dunia, kwa kuratibiwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa chini ya Uongozi wa mtaalam mshauri
kutoka nchini Ghana Seth Vordzorgbe, imewahusisha wataalamu kutoka
katika ngazi ya wizara, mkoa na wilaya pamoja na wadau wa sekta binafsi
na mashirika yasiyo ya kiserikali.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...