Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya- Idara Kuu ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Prudence Constantine na kushoto ni Afisa Maendeleo yaJamii Mkuu Bw. Erasto Ching’oro (kulia) akiongea na waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani kwa mwaka 2020 jijini Dar es salaam leo hii.
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya- Idara Kuu ya maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Prudence Consntatine na kushoto ni Afisa Maendeleo yaJamii Mkuu Bw. Erasto Chingoro (kulia) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na
waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya Siku ya wanawake Duniani kwa mwaka 2020 katikakikao kilichofanyika Jijini Dar es salaam leo hii.
Baadhi ya wanahabari wakifuatailia maelezo ya Wizara ya Afya– Idara Kuu ya Maendeleo yaJamii kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika kitaifa mkoani Simuyutarehe 8 Machi, 2202.

*******************************

Na Mwandishi wetu Dar es salam

Serikali imeitaka jamii kuhakikisha inapinga ukatili wa aina zote ili kufikia malengo ya kuwa na kizazichenye usawa kati ya wanawake na wanaume.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara yaAfya, Idara kuu ya maendeleo ya jamii Bw. Prudence Constantine mapema leo tarehe 21 Februari, 2020jijini Dar es Salaam, amesema kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machimwaka huu kauli mbiu imelenga kutengeneza jamii yenye usawa kati ya mwanaume na mwanaume.

”Katika miaka ya 1990 wanawake walikuwa wanafanya kazi nyingi, ujira kidogo, unyanyasaji,hawakupewa kipaumbele ikilinganishwa na wafanyakazi wanaume” amesema Prudence. Amesema lengo la maadhimisho ya siku hiyo ni kutathmini utekelezaji wa afua za kufikia usawa wa
jinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi, kijamii, kisiasa katika kufikia maendeleo jumuishi.

Maadhimisho haya pia yanatoa fursa ya kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa najamii, Serikali, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na wadau wengine katika kukuza hali ya mwanamke wakitanzania. Kadhalika, katika kuadhimisha Siku hii wadau wanapata fursa ya kubainisha upungufu nambinu za utatuzi wa changamoto zilizopo.

Bw. Prudence amesema Serikali imeendelea na jitihada za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwakuanzisha mfuko wa uwezeshaji kiuchumi ikiwa ni pamoja na mfuko wa maendeleo ya wanawake wenyemasharti nafuu ambao umesaidia kutoa mikopo nafuu na mafunzo ya stadi za biashara kwa wajasiriamaliwanawake.

“Wizara inahakikisha kutumia maadhimisho haya kwa kuandaa makongamano na majukwaambalimbali ili kujadili na kuibua kero zinazokwamisha maendeleo na Ustawi wa wanawake na
kuyatafutia ufumbuzi ikiwemo matatizo ya maji na uchumi duni” amesema Bw. Prudence.

Ameongeza kuwa tangu mwaka 2015/16 hadi 2018/19 Serikali imetoa fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 28.8ambayo imesaidia vikundi vya wanawake 13,691 na kufanya idadi ya wanawake wajasiriamaliwalionufaika na fedha hizo kufikia 883,724 ukilinganisha na wanawake 12,842 kwa mwaka 2013/14.

Aidha, Serikali imewezesha wanawake wajasiriamali kushiriki katika maonesho ya biashara mbalimbaliza Kitaifa na Kimataifa kwa mwaka 2017/18 ambapo wanawake wajasiriamali 1,183 kutoka katika Mikoayote 26 wamenufaika na fursa hiyo kushiriki.

Naye Afisa maendeleo ya jamii Mkuu kutoka wizara ya Afya idara kuu ya maendeleo ya jamiiamebainisha kilele cha maadhimisho kitakuwa na mabanda ya huduma na maonesho ya bidhaa kutoka kwa wanawake wajasiriamali na wadau mablimbali ili kuonesha kazi zinazofanywa na wanawake katikakujiletea maendeleo jumuishi. Kadhalika, kutakuwa na shuhuda za wanawake jasiri ambao wanafanyakazi zilizodhaniwa kuwa ni za wanaume ili kuhamasisha wazazi na wasichana kufanya kazi za aina zote.

Kuelekea maadhimisho hayo pia, kutakuwa na msafara wa kutokomeza ukatili wa kijinsia utakaopitakatika maeneo ya mikoa kadhaa hapa nchini ili kuhimiza upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamiikwa wanawake. Huduma hizi ni pamoja na upimaji wa afya ya akinamama, elimu ya biashara naujasiriamali, kupinga ukatili wa kijinsia, msaada wa kisheria, mabadiliko ya tabia nchi na ushiriki wajamii katika nafasi za uwakilishi na vyombo vya kutoa maamuzi.

Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Kitaifa yatafanyika Mkoani Simiyu tarehe 08 Machi, 2020na kauli mbiu ni “Kizazi cha usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na baadaye” inayosisitizakuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa uwepo wa usawa wa kijinsia katika kufikia malengo ya maendeleoendelevu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...