Charles James, Michuzi TV

ILI kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2020/2021 Jiji la Dodoma limebuni njia saba za ukusanyaji ikiwemo kuwatumia watendaji wa kata na mitaa ili waweze kukusanya mapato katika maeneo yao.

Njia nyingine ni pamoja na kufanya uchambuzi wa vyanzo vya mapato vya halmashauri ili kukusanya takwimu sahihi za vyanzo hivyo, kuhakikisha ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo na vituo vyote unatumia mfumo wa kielektroniki ili kudhibiti upotevu wa mapato.

Akizungumza katika baraza la madiwani wakati wa uwasilishaji mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema mkakati mwingine ni kuboresha minada ya Mpunguzi, Kikombo na Hombolo.

Amesema pia watakua wanaandaa 'database' ya viwanja vyote vinavyozalishwa ili kudhibiti utoaji/ulipaji na uendelezaji, kuandaa mfumo wa ufuatiliaji wa majalada yote ya halmashauri ikiwemo yanayohusu mapato pamoja na kufanya tathimini ya madeni ambayo halmashauri inadai ili kuongeza mapato.

Mikakati hiyo imekuja baada ya mapato ya Jiji hilo lilikoshika namba mbili kwa ukusanyaji wa mapato huku likiongoza kwa mapato ghafi kupungua kutoka kukusanya Sh Bilioni 177 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 hadi Sh Bilioni 116 kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Kunambi amesema kwa mwaka huu wako fedha Jiji la Dodoma limekadiriwa kukusanya mapato jumla ya Sh Bilioni 116 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani (own source), Serikali Kuu, wahisani mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo, utoaji huduma na kujiendesha.

Amesema sababu za kupungua huko kwa mapato kumetokana na kupungua kwa vyanzo vya mapato ya nje na ya ndani. Vyanzo vya mapato ya nje ni ruzuku toka serikali Kuu na kutoletewa fedha toka kwa wahisani kwa miradi ya TSCP, TASAF, SEDEP na EQUIP.

" Mapato ya ndani yamepungua kutokana na kupungua kwa mapato yanayotokana na Idara ya Ardhi, Mipangomiji na Maliasili ambapo kwa mwaka wa fedha ulioisha walikadiriwa kukusanya asilimia 30 ya bajeti yote lakini kwa mwaka huu wako fedha imekusanya asilimia 26 ya bajeti yote.

Lakini sasa tunaamini kwa mikakati tuliyojiwekea tunaenda kufanya vizuri tena kwenye ukusanyaji, tumejipanga kuhakikisha hakuna mapato yatakayopotea," Amesema Kunambi.
 Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akisoma mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2020 kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichokutana leo jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichokaa leo kwenye ukumbi wa Manispaa jijini hapa. Katika kikao hicho baraza la madiwani limepitisha bajeti ya Jiji hilo yenye jumla ya Sh Bilioni 116.
 Madiwani kutoka kata 41 za Jiji la Dodoma pamoja na wataalamu kutoka Idara mbalimbali za jiji hilo wakifuatilia kikao cha baraza la madiwani kilichoketi leo jijini hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...