Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha Jiji la Dodoma linaendana na hadhi ya Makao Makuu ya Nchi, Wakala wa Barabara za vijijini na mijini Tanzania TARURA) jijini humo limepanga kutengeneza na kufanyia marekebisho miundombinu ya barabara ili kuondoa changamoto wanazokutana nazo wananchi.

Hayo yamesemwa na Meneja wa TARURA jiji la Dodoma, Eng Geofrey Mkinga wakati akiwasilisha mpango na bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwenye kikao cha baraza la madiwani.

Eng Mkinga amesema TARURA imepanga kutengeneza na kukarabati kilomita 333.20 na vivuko sita kwa gharama ya Sh Bilioni 4.397.

Ukarabati huo utazingatia matengenezo ya kawaida yatakayogharimu Sh Milioni 368.75, matengenezo kwenye maeneo korofi gharama zikiwa Sh Milioni 588.3, matengenezo maalum gharama zikiwa Sh Milioni 2,410.0 sambamba na vivuko.

Amesema TARURA katika jiji la Dodoma ulikua unahudumia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 781.28 zinazotambulika kisheria mpaka Septemba 2019 ambapo mtandao ulihakikiwa na na kufika urefu wa kilomita 1,179.95.

" Mtandao huu wa barabara utakua ukiongezeka kadri ya upimaji na uendelezaji wa mji unavyoendelea ambapo hadi sasa zaidi ya kilomita 500 za maeneo yaliopimwa bado hayajahakikiwa na kutambuliwa na sheria ya barabara.

Kuhusu vyanzo vya fedha za matengenezo na hali ya barabara amesema wakala unapata fedha za matengenezo ya barabara kutoka vyanzo vikuu vitatu, mfuko wa barabara (road fund), Halmashauri ya Jiji na wadau mbalimbali wa maendeleo, " Amesema Eng Mkinga.

Amesema hali ya barabara kwenye Jiji la Dodoma kwa sasa siyo ya kuridhisha kwa baadhi ya maeneo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyeesha lakini wakala huo umejipanga kufanya matengenezo ili kuondoa kero na changamoto wanazopata watumiaji wake ambao wengi ni wananchi.

Kuhusu mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Eng Mkinga amesema jumla ya Sh Bilioni Nne kutoka bodi ya mfuko wa barabara zimetengwa kugharamia matengenezo ya barabara zenye jumla ya urefu wa kilomita 332 ambazo ni sawa na asilimia 28 ya mtandao wa barabara ndani ya Jiji la Dodoma.
 Meneja wa TARURA Jiji la Dodoma akiwasilisha mpango wa bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwenye kikao cha baraza la madiwani leo.
 Madiwani kutoka kata mbalimbali 41 zilizopo ndani ya Jiji la Dodoma wakifuatilia wasilisho la mpango na bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2020/2022 uliowasilishwa na Meneja wa TARURA, Dodoma Jiji, Eng Geofrey Mkinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...