Na Woinde Shizza,Arusha
WAJUMBE wa Kamati ya Siasa katika Wilaya ya Kichama Arumeru, wameipongeza Halmashauri ya Arusha kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo, walipofanya ziara ya kukagua miradi katika tarafa ya Moshono, ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi( CCM).
Wajumbe hao, wameonesha wazi kuridhishwa na ubora wa miradi waliyoikagua, na kuthibitisha mapinduzi makubwa ya kimaendeleo yaliyofanyika hasa katika maeneo ya vijijini, kwa kipindi kifupi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya tano, inayoongizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM wilayani Arumeru Simon Ole Saning'o, amekiri mapinduzi hayo makubwa ya kimaendeo, yanayoonekana wazi kupitia utekelezaji wa kasi wa miradi ya Maendeleo kisekta.
Saning'o amekiri mpaka sasa Serikali ya Awamu ya Tano, imetekeleza Ilani ya CCM kwa zaidi ya asilimia 90, ikiwa imejikita zaidi kutekeleza miradi mikubwa katika sekta za elimu, afya, maji, umeme, pamoja na Miundombinu ya barabara. "Rais Magufuli, ilipoingia madarakani, alikabidhiwa ilani ya CCM, iliyojikita kwenye kuendeleza sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara, Umeme na Kilimo, kwa kipindi kifupi cha miaka minne, Serikali imefanya mapinduzi makubwa, katika utekelezaji wa Ilani, tofauti na vipindi vilivyopita,"amesema Mwenyekiti Saning'o"
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, shule ta sekondari sokoni II, uliogharimu shilingi milioni 190 kupitia ubalozi wa Japan, ujenzi wa maktaba na ukarabati wa bwalo sekondari Mlangarini milioni 140 fedha za EP4R , ujenzi wa darasa shule ya sekondari Olokii kwa nguvu za wananchi , ujenzi wa Kituo cha Afya Nduruma milioni 500 Serikali Kuu, ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo shule ya Msingi Lameloku milioni 60 fedha za Miradi ya TASAF
Ziara hiyo ilimalizika kwa wajumbe hao wa kamati, kuzungumza na wananchi wa Kata ya Bwawani katika mkutano wa hadhara, uliofanyika kijiji cha Lameloku na kufanikiwa kujadili mikakati na changamoto mbalimbali zinazokabili utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata yao, huku kamati hiyo ikiwapongeza wananchi kwa kushiriki kwa vitendo, kuunga mkono juhudi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...