Na Woinde Shizza,Arusha
SHIRIKA la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii( NSSF) Mkoa wa Arusha limewafikisha mahakamani waajiri 34 ambao ,wadaiwa sugu kutoka kampuni mbalimbali mkoani hapa ,wakidaiwa kiasi cha zaidi ya Sh.bilioni 7.16.
Akizungumza na vyombo vya habari mapema ofisini kwake, Meneja wa NSSF mkoani hapa, Juma Mwita amesema shirika hilo limefikia hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa kampuni hizo zimeshindwa kuwasilisha michango ya wanachama kwa muda mrefu licha ya hatua ya majadiliano mbalimbali kufanyika.
"Sheria inaelekeza kila mwajiri kuhakikisha anawasilisha michango ya wafanyakazi wake kwa wakati ila kwa baadhi ya waajiri wameshindwa kutii sheria hilo sisi kama shirika tumeona njia sahihi ni kutumia mahakama" Amesema
Aidha ameongeza kuwa waajiri hao wamesababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyakazi wao licha ya wanachama kuchangia lakini waajiri wamekuwa wagumu kuwasilisha michango yao jambo ambalo kama shirika tumeona ni ukiukwaji wa sheria.
Amesema katika kiasi hicho cha fedha baadhi ya waajiri zikiwemo kampuni za ukandarasi wameanza kuonyesha nia ya kupunguza madeni kwani hadi sasa kiasi cha shilingi milioni 400 kimelipwa kati ya sh,bilioni 7.16 wanazodai.
Amezitaja baadhi ya kampuni zinazodaiwa madeni makubwa kuwa ni pamoja na chuo cha Mount Meru,Kijenge Animal, Pride Tanzania,Tanzania One Mining.
Amesema NSSF Mkoa wa Arusha linazaidi kampuni 2200 yenye wanachama wanaochangia ila miongoni mwa makampuni hayo yameshindwa kuwasilisha michango ya wanachama wao na kufikia deni za zaidi ya bilioni 7.
Mwita amewaonya baadhi ya waajiri ambao wamekuwa hawawasilishi michango ya wanachama kwa wakati kuwa, watachukuluwa hatua Kali kwa kufikishwa mahakamani kwani wanawanyima haki stahili za wanachama wachangiaji .
Amesema kuwa taratibu zinaelekeza kuwa mwajiri asiye wasilisha michango ya wanachama ndani ya miezi sita atachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...