Kampuni ya Agrocom Africa imeendesha mafuzo kwa wafanyakazi wake, juu ya namna ya matumizi sahihi ya Trekta mpya na za kisasa za Kampuni ya Kubota kutoka nchini Japan, ambazo zitaanza kuuzwa na kampuni hiyo hapa nchini, ambapo wafanyakazi hao waliweza kupata mafunzo ya darasani na kwa vitendo pia. Pichani ni Mkufunzi kutoka Kampuni ya Kubota, Kazunori Sasaki akitoa mafunzo hayo, yaliyofanyika kwenye Tawi la Agricom, Melela Mkoani Morogoro leo.
 Mmoja wa Mafundi wa Kampuni ya Kubota ya nchini Japan, Hiroshi Iwashita akiwaonyesha baadhi ya Wafakazi wa Kampuni ya Agrocom namna Betri ya Trekta aina Kubota L 4508 inavyotakiwa kufungwa, wakati wa mafunzo maalum ya matumizi ya Trekta hizo, yaliyoandaliwa na Kampuni ya Agrocom Africa.
 Muonekano wa Trekta mpya aina ya Kubota L 4508 za nchini Japan, zikiwa tayari kwa kazi mbalimbali za kilimo.
 Baadhi ya Mafundi na Wafanyakazi wa Kampuni ya Agrocom Africa, wakiwa katika mafunzo ya vitendo.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...