Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

BAADA ya siku tatu tangu Mamlaka ya upelelezi nchini Rwanda kutangaza kumshikilia mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini humo Kizito Mihigo kwa tuhuma za kujaribu kuvuka mpaka na kwenda kujiunga na vikosi vinavyopinga Serikali ya Rwanda pamoja na kushutumiwa kwa vitendo vya rushwa leo Februari 17 jeshi la polisi nchini humo limetangaza kuwa maiti ya Kizito imepatikana ndani ya chumba alichokua amezuiwa  katika kituo cha polisi cha Remera mjini Kigali.

Polisi wamesema kuwa Kizito amejinyonga baada ya kukamatwa karibu na mpaka wa Rwanda na Burundi huku wakieleza kuwa alidhamiria kutoroka nchini humo na kujiunga na makundi ya waasi dhidi ya Serikali ya Rwanda.

Mamlaka za uchunguzi zimesema kuwa uchunguzi kufuatia kifo chake umeanza na hiyo ni pamoja na kupeleka mwili wake katika chumba cha kuhifadhia maiti ambapo uchunguzi utafanywa huku taarifa za awali zikieleza kuwa Kizito amejinyonga leo alfajiri kwa kutumia nguo aliyokuwa analalia.

Licha ya taarifa hiyo kutolewa baadhi ya wanaharakati wamepinga taarifa hizo na kueleza kuwa mwanamuziki huyo hakutaka kutoroka kwenda kujiunga na kundi la waasi huko Burundi ila alitaka kwenda nchini Ubelgiji alipokuwa akiishi.

Wengi wa wanaharakati hao wamesisitiza kuamini kwamba Kizito hakujiua ndani ya chumba katika kituo cha polisi alipokuwa anazuiliwa na kwamba huenda aliuawa.

Kifo cha Kizito kimeelezwa kusababisha na muziki wake aliotoa kuhusiana na mauaji ya Kimbari 1994 ambapo mwaka uliopita aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuhamasisha wananchi kupinga Serikali na  kutaka kumuua Rais Paul Kagame.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...